Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Habari Siasa CCM, UKAWA watafunana Muswada wa Vyama vya Siasa
SiasaTangulizi

CCM, UKAWA watafunana Muswada wa Vyama vya Siasa

Spread the love

WABUNGE kutoka chama tawala- Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale kutoka vyama vya upinzani wameanza kumenyana kuhusu Muswada mpya wa Vyama vya Siasa uliowasilishwa bungeni leo tarehe 29 Januari 2019. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Wabunge kutoka CCM wanadai kuwa, wabunge wa upinzani wanahofu na vipengele vilivyomo kwenye muswada huo kutokana na ‘madhambi’ yao huku upinzani ukieleza kuwa, kuna vipengele vinavunja Katiba ya Nchi.

Halima Mdee, Mbunge wa Kawe (Chadema) akichangia bungeni muswada huo amesema, CCM imekuwa ikipotosha kuhusu msimamo wa wapinzani kuhusu muswada huo.

Amesema, wapinzani hawaogopi kukaguliwa na kwamba, serikali ilipaswa kuwa na woga huo kwa kuwa, karibu miaka yoye taasisi nyingi za serikali zinapata hati chafu kutokana na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Amesema, Kamati ya Katiba na Sheria imeondoa baadhi ya vipengele na kwamba, vipo vilivyobakizwa ambavyo bado vinaweka ukakasi katika muswada huo.

Mdee amekumbusha wabunge wa CCM kwamba, wao ndio waliokuwa wakipinga kuwepo kwa ukaguzi ndani ya vyama vyao na kwamba, msajili anaongezewa majukumu ambayo anaweza kuepushwa nayo.

Mbunge huyo wa Kawe amewaonya CCM kusimamia kuvunjwa kwa Katiba ya Nchi kutokana na baadhi ya vipengele kutokana na kunyima uhuru wa kufanya siasa kwa mujibu wa katiba yenyewe. Ametaja kifungu cha 8 (c) ndani ya Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Sheria ya mwaka 2018 kinavunja Katiba.

Wakati Mdee akituhumu CCM, Joseph Mhagama, Mbunge wa Madaba (CCM) ametaka Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni kuacha upotoshaji juu ya muswada huo.

Mhagama amesema, muswada huo unalenga katika kuweka uwazi na uwajibikaji katika uendeshaji wa vyama vya siasa.

“Suala la uwajibikaji unaona katika muswada huu ambao unataka vyama vyote vitoe tamko ya mali na madeni ya taasisi zao. Ibara 22 inaitaka vyama vya siasa viwe na ofisa masuhuli,”amesema.

Amesema, katika Ibara ya 23 ya muswada huo kwenye utekelezaji wa dhana ya uwazi na uwajibikaji, inataka vyama vya siasa iwe na akaunti maalum ya kuhifadhi fedha za ruzuku na kwamba, pia muswada huo unataka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua hesabu za vyama.

“Watanzania wajue kuwa, wenzetu ambao walikuwa wakiendesha vyama vya siasa kwa mfumo wa ukanjanja, udanganyifu. Wenzentu wamekuwa wakitumia vyama vya siasa kama sio taasisi za kwenda kuijenga nchi isipokuwa kama Saccos (Vyama vya kuweka na Kukopa),”amesema na kuongeza;

“Vyama vya siasa ni matanuru ya kupika viongozi wakishaiva ndio wanakwenda kuongoza nchi. Haki na wajibu ni kujiridhisha juu ya maudhui yanayokwenda katika vyama vya siasa ili yaendane na utamaduni, mila na desturi za kitanzania,”amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!