January 16, 2021

Uhuru hauna Mipaka

CCM kutangaza ‘hasimu’ wa Maalim Seif urais Z’bar

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), leo tarehe 10 Julai 2020, kinatarajia kumtangaza mgombea urais wake visiwani Zanzibar. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mgombea huyo ndiye atakayepambana na mwanasiasa nguli visiwani humo, Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye tayari amechukua fomu ya kugombea ngazi hiyo ndani ya chama chake cha ACT-Wazalendo.

Maalim Seif, makamu mwenyekiti wa chama hicho amekuwa mgombea urais visiwani humo katika vipindi vitano mfululizo, mara zote hizo amelalamika kuporwa ushindi wake na CCM. Tayari ametoa tahadhari kwenye uchaguzi wa mwaka huu, kwamba akiporwa ‘hatozuia hasira za Wazanzibari.’

           Soma zaidi:-

Mgombea wa CCM anatarajiwa kupatikana leo baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kufanya kikao cha kuchagua jina moja la mwanachama wake, ni kati ya majina matano ya watia nia yaliyopitishwa na Kamati Maalum ya NEC.

Jumamosi ya tarehe 4 Julai 2020, Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, ilipendekeza majina matano ya watia nia kugombea Urais wa Zanzibar kati ya 31 waliojitokeza, kwa NEC.

“Tarehe 10 Julai 2020, kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kitachagua jina moja la mwanachama atakayesimama kugombea Urais wa Zanzibar,” inaeleza ratiba ya CCM.

Baada ya NEC kuteua jina hilo, Mkutano Mkuu wa CCM Taifa utakaofanyika kesho Jumamosi tarehe 11 hadi 12 Julai, 2020, utathibitisha jina la mwanachama atakayesimama katika Uchaguzi wa Urais wa Zanzibar.

error: Content is protected !!