January 24, 2021

Uhuru hauna Mipaka

CCM haininyimi usingizi Mafia – Mngwali

Riziki Mngwai, mtia nia wa ubunge katika Jimbo la Mafia kupitia Chama cha ACT-Wazalendo

Spread the love

RIZIKI Mngwali, mtia nia wa ubunge katika Jimbo la Mafia kupitia Chama cha ACT-Wazalendo amesema, kelele za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye jimbo hilo hazimnyimi usingizi. Anaripoti Hamis Mguta, Mafia … (endelea).

Amesema, mwisho wa siku Mungu ndiye huamua nani awe mbunge katika jimbo gani, na kwamba hata CCM na watu wao watandike kadi barabarani ‘kama imeandikwa itakuwa kama ilivyoandika.’

Mngwali ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maaalum Mafia, alitoa kauli hiyi jana tarehe 7 Julai 2020, katika ofisi za ACT-Wazalendo Wilaya ya Mafia baada ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge wa jimbo hilo.

“CCM hawaninyimi usingizi maana nguvu yao ni ndogo hapa Mafia,” amesema Mngwali akijibu swali la mwandishi kuhusu maandalizi yake ya kuwania jimbo hilo.

“Mimi kama Mungu kanipangia kuwa Mbunge wa Mafia wa jimbo, kupitia ACT-Wazalendo nitakuwa hata kama CCM watatandika kadi zao hadi kando ya barabara,” amesema Mngwali.

Amesema, amekuwa akipigiwa simu na baadhi ya watu wakimkatisha taama ya uamuzi wake kwa kugombea jimbo hilo, “eti wanasema nitafanyiwa mkakati ili nisishinde, hilo kwani halinirudishi nyuma.”

Mngwali ni miongoni mwa wabunge wanane pamoja na madiwani wawili waliofukuzwa uanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) mwaka 2017, kwa madai mbalimbali ikiwemo ukosefu wa nidhamu ndani ya chama.

Wabunge waliofukuzwa CUF ni Miza Haji, Saverina Mwijage, Salma Mwasa, Raisa Mussa, Hadija al Qassim, Halima Mohamed, Saumu Sakala, madiwani ni Elizabeth Magwaja na Layla Madibi.

error: Content is protected !!