January 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Cavani kuiongoza Man Utd dhidi ya Chelsea

Spread the love

MSHAMBULIAJI mpya wa klabu ya Manchester United Edson Cavani ataiongoza safu ya ushambuliaji ya Manchester United kwa mara ya kwanza dhidi ya Cheksea kwenye mchezo wa Ligi Kuu nchini England leo tarehe 24 Oktoba, 2020. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Mchezo wa mzunguko wa kwanza kwenye Ligi Kuu nchini humo utapigwa majira ya saa 1 usiku kwenye Uwanja wa Old Traford jijini Manchester.

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa mchezaji huyo hakuwa timamu ‘fit’ kwenye michezo miwili iliyopita kutokana na kukaa mbali na mpira kwa muda mrefu, lakini sasa anaonekana yupo sawa kuwakabili Chelsea.

“Hakuwa yupo tayari kwa mchezo dhidi ya PSG kwa sababu ilikuwa mapema sana kwake, hakuwa amefanya mazoezi ya kutosha lakini ameweza kufanya hivyo wiki na kuonekana yupo tayari kwa mchezo dhidi ya Chelsea,” alisema kocha huyo. 

Mchezaji huyo ambaye alijiunga na Manchester United katika dirisha kubwa la usajili kama mchezaji huru mara baada ya mkataba wake na klabu ya PSG kumalizika.

Cavani amefunga jumla ya mabao 341 kwenye michezo 556 aliyocheza kwenye klabu tofauti alizopitia kwenye maisha yake ya mpira.

Manchester United inaingia kwenye mchezo wa leo dhidi ya Chelsea ikiwa nafasi ya 15 baada ya kushinda michezo miwili kati ya minne waliocheza kwenye Ligi Kuu nchini humo.

error: Content is protected !!