Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge Tanzania lafanya mabadiliko makubwa ya kanuni
Habari za SiasaTangulizi

Bunge Tanzania lafanya mabadiliko makubwa ya kanuni

Bunge la Tanzania
Spread the love

BUNGE la Tanzania, limepitisha mabadiliko makubwa ya kanuni zake ambazo zitaanza kutumika katika Bunge la 12 ikiwemo kubadili jina la Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na kiapo kwa wabunge. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mabadiliko hayo, yamewasilishwa leo Jumatatu tarehe 15 Juni 2020 bungeni jijini Dodoma na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson.

Bunge hilo la 11 linalooongozwa na Spika Job Ndugai lililozinduliwa tarehe 20 Novemba 2015 na Rais wa Tanzania, John Magufuli, kesho Jumanne atalihitimisha kwa kulihutubia.

Akiwasilisha mapendekezo hayo, Dk. Tulia amesema, kumekuwapo na wabunge na wajumbe wanaowakilisha Bunge katika mabunge duniani kama Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Bunge la Jumuiya ya Madola (CPA).

Amesema, kumekuwa hakuna, utaratibu wa kumwita au kumrejesha nchini mbunge au mjumbe anayewakilisha Bunge katika vyombo vya uwakilishi kwani, “pamoja na Bunge kuwachagua kuwawakilisha, lakini kanuni za Bunge hazijaweka masharti ya kumrejesha” kama atakuwa mgonjwa, amekuwa na mwenendo usiofaa ana unadhalilisha nafasi anayoitumikia au kutetea na kuzingatia maslahi ya nchi yake.

Dk. Tulia amesema, ili kupatikana kwa suluhisho la matatizo hayo, kuwepo na kanuni za kumrejesha nchini ili aweze kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Mabadiliko mengini yanahusu makosa ya kinidhamu ambapo Dk. Tulia amesema, katika kipindi cha Bunge la 11 kumekuwapo na makosa makubwa ya kinidhamu na vitendo hivyo vimekuwa vikijirudiarudia.

Amesema kutokana na hilo, Dk. Tulia amesema, utovu wa nidhamu, kosa hili litachukuliwa kama kosa dogo iwapo mbunge kutishia kutumia nguvu ndani ya Bunge au katika vikao vya kamati za Bunge.

Amesema, mbunge anayetenda kosa la nidhamu aadhibiwe na spika kwa kupewa onyo au kutolewa nje ya Bunge au kusimamishwa kuhudhuria vikao visivyozidi kumi vya Bunge.

Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson

Dk. Tulia amesema, kosa kubwa la utovu wa nidhamu, lichachukuliwa kama kosa kubwa na mfano, Bunge kudharau uamuzi wa Spika, kusababisha vurugu ndani ya Bunge na kurejea kosa alilokosea.

Pia, kukataa kuomba radhi au kufuta maneno yasiyo ya kibunge bungeni, kujaribu kuvuruga msafara wa spika anapoingia au kutoka bungeni na kupiga kura mara mbili katika jambo la uamuzi bungeni.

“Mbunge anayetenda kosa kubwa la nidhamu, asimamishwe vikao visivyopungua 15 iwapo ni kosa la kwanza au kusimamishwa vikao visivyozidi 20 kama ni kosa la pili au adhabu yoyote iliyopendekezwa na kamati ya maadili,” amesema Dk. Tulia.

Dk. Tulia amesema, utovu wa nidhamu uliokithiri ni kujaribu kumshambulia spika au mgeni bungeni, kuondoa siwa bungeni, kusababisha vurugu bungeni zinazoweza kusababisha mkutano wa Bunge kuahirishwa.

“Mbunge aliyetenda kosa la nidhamu uliokithiri kwanza ni kusimamishwa kuhudhuria mikutano isiyopungua miwili na isiyozidi mitatu.”

“Adhabu nyingine itakayopendekezwa na kamati au Bunge liazimie kwamba shauri hilo lishughulikiwe kwa mujibu wa sheria za maadili za viongozi wa umma ambapo mbunge husika anaweza kupewa adhabu ya kufukuzwa ubunge,” amesema Dk. Tulia. 

Vurugu Bungeni

Katika mabadiliko hayo, Dk. Tulia amesema, utaratibu wa kushughulikia mapendekezo ua mpango wa muda mrefu.

Amesema, utaratibu uliopo ni Bunge kujadili mpango wa muda mrefu lakini mapendekezo ya mpango wa muda mrefu haukuwepo lakini sasa utakuwa unajadiliwa na mkutano wowote wa Bunge.

Dk. Tulia amesema, mabadiliko mengine ni kuboresha utaratibu wa kushughulikia malalamiko dhidi ya uamuzi wa Spika kwa kuweka ukomo wa muda, “Inapendekezwa mbunge awasilishe malalamiko yake kwa katibu wa bunge ndani ya siku moja tangu uamuzi ulipotolewa.”

Mabadiliko mengine, Dk. Tulia amesema, kuboresha kwa kubadili jina la Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, “Inapendekezwa kambi ya wabunge ambao vyama vyao haviundi Serikali ijulikane kama ‘Kambi Rasmi ya Waliowachache’ badala ya kambi ya upinzani bungeni.”

“Ili kuendana na utamaduni wa baadhi ya mabunge ya Jumuiya ya Madola kama vile Kenya. Hii itasaidia kuondoa dhana ya wabunge wa kambi hiyo kupinga kila kitu kinacholetwa na serikali badala ya kutoa mawazo mbadala na yenye tija kwa taifa,” amesema.

Dk. Tulia amebainisha mabadiliko mengine ya kanuni hizo ni, kuboresha kiapo cha mbunge kwa kuondoa neno “utii” kwenye kiapo cha mbunge na kuweka neno “uaminifu” ambalo lipo kwenye Katiba na sharia za viapo kwa viongozi.

“Pili, kuweka utaratibu wa mbunge mteule wa Rais na mbunge anayeshinda katika uchaguzi mdogo, kuapishwa mara moja ili kuanza kutekeleza majukumu yake bila kusubiri Bunge kukutana na spika atatoa taarifa bungeni kuhusu mbunge aliyeapishwa na kujitambulisha,” amesema Dk. Tulia.

Katika mabadiliko mengine, Dk. Tulia amesema, kuwasilisha jina la mbunge anayependekezwa na Rais kushika nafasi ya waziri mkuu itakavyomfikia spika, “inapendekezwa taarifa hiyo iwasilishwe na mpambe wa rais au mtu yoyote atakayetumwa na rais ili imfikie Spika.”

Kuhusu muda wa kuzungumza Bungeni, Dk. Tulia amesema, kutokana na ongezeko la wabunge bungeni na kuchangia, wamependekeza muda wa kuchangia umepunguzwa kutoka dakika 15 hadi 10, muda wa waziri kuhitimisha hoja kutoka dakika 60 hadi 30, muda wa upinzani kuwasilisha maoni kutoka dakika 30 hadi 15.

Dk. Tulia ametangaza mabadiliko mengine ya kuboresha masharti ya malipo ya mshahara na posho kwa mbunge aliyemahabusu na anayetumikia kifungo, “mbunge aliyemahabusu kulipwa nusu mshahara na posho zinazoambatana na mashara wake, mbunge anayetumikia kifungo kutolipwa posho au mshahara.”

“Msingi wa mapendekezo hayo ni mbunge kutofanya kazi ya mbunge kwa wakati huo anapotumikia adhabu,” amesema Dk. Tulia.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika majukumu yao katika moja ya kumbi za Bunge

Pia, Dk. Tulia amesema, kuboresha utaratibu wa ukusanyaji na utoaji wa habari za Bunge kwa kueleza misingi ya ukusanyaji na utoaji wa habari, matangazo ya moja kwa moja ya mikutano ya Bunge kurushwa na Studio ya Bunge.

“Masharti ya upigaji picha ya bunge, inapendekezwa chombo au mwandishi wa habari atakayekiuka masharti apewe onyo, kusimamishwa kuchukua au kutoa habari za Bunge au kufutiwa kibali cha kufika bungeni,” amesema.

Baada ya kumaliza kuwasilisha mapendekezo hayo yaliyoandaliwa na kamati ya Bunge ya kanuni iliyoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, wabunge walichangia kisha zikapitishwa.

Spika Ndugai amesema, kanuni hizo zitaanza kutumika katika mkutano wa Bunge wa 12 utakaokutana Novemba 2020 baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu Oktoba 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

error: Content is protected !!