Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge lamhoji Prof. Assad kwa saa nne 
Habari za SiasaTangulizi

Bunge lamhoji Prof. Assad kwa saa nne 

Prof. Mussa Assad, Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) akiwa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili, Hadhi na Madaraka ya Bunge
Spread the love

PROF. Mussa Assad, mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali (CAG), amemaliza kuhojiwa na Kamati ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge. Mahojiano yalichukua takribani saa nne. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Prof. Assaad aliingia ndani ya Kamati hiyo, saa 4:47 asubuhi. Alitoka saa 8:48 mchana.

Haikuweza kufahamika mara moja, nini kilijadiliwa katika kikao hicho.

MwanaHALISI Online lilipomuuliza Prof. Asaad juu ya kilichojadiliwa, haraka alisema, “hapana. Sina la kusema.”Prof. Assad amekuwa kwenye mvutano na Bunge, mara baada ya kunukuliwa akiwa nchini Marekani akisema, hatua ya mhimili huo wa kutunda sheria na kusimamia serikali, kushindwa kufanyia kazi ripoti za ukaguzi za fedhaoinazoibuliwa na ofisi yeke, “ni sawa na udhaifu.”

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, Emmanuel Mwakasaka amesema mahojiano na CAG yalienda vizuri.

“Kama mnavyojua CAG aliagizwa kufika kwenye kamati ya hii ili kuhojiwa na kudhibitisha maneno yake na kweli amefika saa tano kamili kimsingi amejieleza kwa kutupatia ushirikiano mzuri sana.
“Hamefika tumemhoji na amejibu kwa kutoa ushirikiano mkubwa kwa kamati,lakini pamoja amekuwa na vielelezo ambavyo tunaendelea kufanya uchunguzi.
“Tumemsikiliza vizuri shahidi (CAG) sisi kwa kanuni zetu hatumuiti mtuhumiwa tunamwita shahidi hivyo ushahidi ukikamilika tutamfikishia Spika ili yeye kwa kuwa ndiye aliyetoa wito kwa sahidi huyo kufika atajua ni nini hatua zifakazofuata,” alisema Mwakasaka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!