Job Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania

Bunge la Tanzania kumpongeza Spika Ndugai

Spread the love

BUNGE la Tanzania, linatarajia kupitisha Azimio la kumpongeza Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai kwa mafanikio ya Bunge la 11. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Kwa mujibu wa orodha za shughuli za Bunge za leo Jumatatu tarehe 8 Juni 2020 zilizotolewa na Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai inaonyesha, miongoni mwa shughuli ni kupitisha “Azimio la Bunge la kumpongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mafanikio ya Bunge la 11.”

Ndugai ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amekuwa Spika wa Bunge la 11 lililozinduliwa rasmi na Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli tarehe 20 Novemba 2015.

Bunge la 11 linatarajiwa kuhitikisha tarehe 19 Juni 2020 kwa Rais Magufuli kutoa hotuba yake ya mwisho.

Baada ya kuvunjwa kwa mujibu wa sheria, kitakachofuata ni nchi hiyo kuingia rasmi kwenye mchakato wa uchaguzi wa madiwani, wabunge na Urais Oktoba 2020.

Ndugai amekuwa Spika wa saba akichukua uongozi huo kutoka kwa Anne Makinda aliyeongoza kati ya Nobemba 2010 hadi Novemba 2015. Wakati huo, Ndugai alikuwa Naibu Spika.

Makinda alimpokea marehemu Samwel Sitta aliyekuwa na falsafa ya ‘Mzee wa kasi na viwango’ aliyeongoza muhimili huo kati ya Desemba 2005 hadi Novemba 2010.

Sitta alikalia kiti cha uspika kutoka kwa Pius Msekwa aliyeongoza Bunge kati ya Aprili 1994 hadi Novemba 2005. Msekwa alipokea kijiti kutoka kwa marehemu Adam Sapi Mkwawa aliyeongoza kati ya Nobemba 1975 hadi Aprili 1994.

Mkwawa yeye alimpokea Erasto Mang’enya aliyeongoza Bunge kati ya Nobemba 1973 hadi Nobemba 1975 alichukua nafasi iliyokuwa imeachwa tena na Adam Sapi Mkwawa kati ya Apruli 1964 hadi Novemba 1973.

Endelea kufulia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV (Youtube) kujua kitakachojili bungeni*

BUNGE la Tanzania, linatarajia kupitisha Azimio la kumpongeza Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai kwa mafanikio ya Bunge la 11. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea). Kwa mujibu wa orodha za shughuli za Bunge za leo Jumatatu tarehe 8 Juni 2020 zilizotolewa na Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai inaonyesha, miongoni mwa shughuli ni kupitisha “Azimio la Bunge la kumpongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mafanikio ya Bunge la 11.” Ndugai ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amekuwa Spika wa Bunge la 11 lililozinduliwa rasmi na Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli tarehe…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!