July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bunge la Marekani lavamiwa, risasi zarindima

Bunge la Marekani

Spread the love

WAFUASI wa Donald Trump, Rais wa Marekani wamevamia bunge la nchi hiyo, jijini Washington wakitaka rais huyo kubaki madarakani. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Uvamizi huo umefanyika wakati kikao cha bunge la seneti kikiwa kimeketi kuidhinisha urais wa Joe  Biden, rais mteule wa Taifa hilo.

Tayari mwanamke mmoja amepigwa risasi na kuuawa huku mwingine akiendelea kupatiwa matibabu kutokana na majeraha ya risasi kifuani.

Biden amelaumu ushawishi unofanywa na Trump kutaka kuwaaminisha baadhi ya raia kwamba, aliibiwa kura kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.

Polisi jijini humo wameeleza, waandamaji hao walikuwa tayari kutumia nguvu ili kuingia katika jengo hilo la Bunge.

Donald Trump

Katika hekaheka za kukabiliana na maandamano, polisi wamekamata silaha tano na watu 13.

Waandamanaji hao walikuwa wakiimba ‘tunamtaka Trump’ huku wengine wakisema ‘hatukubali aondoke.’

Robert Contee, Mkuu wa Polisi Washington  amewaambia wanahabari kuwa, waliokamatwa sio wakazi wa eneo hilo.

Kutokana na uvamizi huo, Trump alirekodi ujumbe wake na kuuchapisha kwenye ukurasa wake wa twitter akiwataka wafuasi wake kurejea majumbani.

Hata hivyo, kwenye ujumbe huo huo aliendeleza madai yake ya kuibiwa kura na kusababisha kushindwa kwenye uchaguzi huo.

Joe Biden, Rais wa Marekani

“Najua machungu yenu, najua mmevunjika moyo lakini lazima sasa mrejee nyumbani, lazima tuwe na amani, hatutaki yeyote ajeruhiwe,” aliandika Trump.

Baada ya ujumbe huo, waandamanaji walipunguza munkari na kuanza kuondoka eneo la bunge hilo.

Maofisa wa polisi na jeshi wamepelekwa jirani na jimbo hilo ili kuhalikisha tukio kama hilo halitokei.

Kutokana na tukio hilo, baadhi ya viongozi duniani wamelaani uvamizi huo.

Boris Jonhson, Waziri Mkuu wa Uingereza

Boris Jonhson, Waziri Mkuu wa Uingereza amekiita kitendo hicho kwamba ni cha aibu.

“Marekani inasimamia demokrasia kote duniani, na ni muhimu sana kuwa na ubadilishanaji wa madaraka kwa njia ya amani na yenye mpangilio,” ameandika kwenye UK u rasa wake wa twitter.

Wazriri wa kwanza wa Scotland, Nicola Sturgeon ameandika kuwa kinachotokea bungeni “kinatia hofu mno.”

Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sánchez amesema “Nina imani na demokrasia ya Marekani. Uongozi wa rais mpya Joe Biden utakabiliana na kipindi hiki kigumu, kuunganisha watu wa Marekani.”

error: Content is protected !!