Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bulaya, Mdee kutupwa sero
Habari za Siasa

Bulaya, Mdee kutupwa sero

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imewataka mshtakiwa Halima Mdee na Ester Bulaya waeleze kwanini wasifutiwe dhamana zao. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Mdee, Mbunge wa Kawe na Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini na viongozi saba wa Chadema, kwenye kesi namba 112/2018 kwa makosa 13, yakiwemo kutoa maneno ya uchochezi, kufanya kusanyiko lisilo halali na maandamano yaliyosababisha kifo cha Akwelina Akwelin, aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Usafirshaji Tanzania (NIT).

Washitakiwa wengine kwenye shauri hilo ni Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema-Taifa; John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini; John Mnyika, Katibu Mkuu wa chama hicho; Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini.

Pia yumo Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini; Salum Mwalim, Naibu Katibu Mkuu- Zanzibar na Vincent Mashinji – mwanachama mwandamizi wa chama hicho.

Leo tarehe 20 mbele ya Thomas Simba, Hakimu Mkazi Mkuu, Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi aliyesaidiwa na Wakiki wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amewasilisha hoja kwamba Bulaya na Mdee wamekiukwa masharti ya dhamana, kwa kuwa wakisafiri nje ya nchi bila kibali cha mahakama.

Nchimbi ameieleza mahakama kuwa, moja ya masharti waliyopewa washtakiwa hao ni kutosafiri nje mipaka ya Tanzania bila kibali cha mahakama.

Nchimbi amedai, upande unataarifa za uchunguzi zinazoonesha kuwa, wiki mbili zilizopita Bulaya na Mdee walionekana uwanja wa ndege wakirejea kutoka Kenya.

Na kwamba, hilo linaonekana katika hati ya kusafiria ya Bulaya yenye namba TBE 011989, na Mdee namba TBE 011991, ambapo aliomba mahakama hiyo, watuhumiwa hao waeleze iwapo walisafiri kwa kibali cha mahakama.

John Mallya, wakili wa utetezi ameieleza mahakama kuwa isipoteze muda wake kusikiliza hoja hizo, hata hivyo hakimu Simba amesema, ipo haja ya watuhumiwa kueleza iwapo walisafiri kwa kibali cha mahamakama.

Mdee ameieleza mahakama hiyo kuwa, hakwenda Kenya bali Afrika Kusini kwa matibabu na kwamba, alipata kibali cha mahakama baada ya daktari wake kutoka Hospitality ya Agha Khan, kuandika barua ya kumuombea ruhusa pia Bulaya kwa ajili ya kumsindikiza.

Bulaya ameeleza mahakama hiyo, kuwa aliruhusiwa kusafiri na Mdee kwa ajili ya kumsindikiza.

Wakati huo huo nchimbi amedai, watuhumiwa wamekiuka masharti ya dhamana na kwamba mahakama iwaite wadhamini wa washitakiwa hao ili waeleze, kwani wadhamana wao walisafiri bila kibali cha mahakama.

“Tarehe 13 Januari 2020, wakili Hekima Mwasipu aliwasilisha ombi mahakamani juu ya kuwaombea washtakiwa wote tisa waende Kenya, lakini tarehe 15 Januari 2020 mahakama iliyakata maombi hayo na hapakuwa na maombi ya kusafiri kwenda Afrika Kusini,” amesema.

Wakili Mallya ameeleza mahakama hiyo kwamba, ombi la jamhuri halina msingi wowote wa kisheria. Hata hivyo, Hakimu Simba amesema, shauri hilo litaendelea kesho tarehe 21 Januari 2020 saa tano asubuhi.

Na kwamba, wadhamini wa Bulaya na Mdee watatakiwa kujieleza sababu za wadhaminiwa wao kusafiri bila kibali cha mahakama na kwanini wasifutiwe dhamana zao.

Awali, mdhamini wa John Mnyika, alieleza mahakama kuwa mdhamana wake alimpigia simu jana tarehe 19 Januari 2020, kuwa amefiwa na baba yake mdogo wilayani Misinyu, Mwanza hivyo amekwenda kwa ajili ya mazishi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!