April 11, 2021

Uhuru hauna Mipaka

BoT yachapisha noti mpya

Benki Kuu ya Tanzania (BoT)

Spread the love

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imezifanyia maboresho fedha za noti, toleo la mwaka 2010, katika kipengele cha usalama. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na BoT tarehe 2 Aprili 2020, fedha hizo ni Tsh. 1,000, 2,000, 5,000 na 10,000.

Maboresho hayo ni pamoja na saini,  ambapo imewekwa saini ya Dk. Phillip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango wa sasa, pamoja na saini ya Gavana wa BoT iliyeko madarakani, Profesa Florens Luoga.

Maboresho mengine ni kamba nyembamba iliyowekwa maelezo ya fedha, ambayo ina picha inayotembea wakati fedha ikigeuzwa juu chini, au upande mmoja kwenda upande mwingine.

Aidha taarifa ya BoT inaeleza kwamba, alama zingine za usalama zitabaki kama zilizvyo, pia fedha hizo zimeshatolewa katika mzunguko wa fedha.

error: Content is protected !!