July 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Bosi Takukuru azungumzia walipofikia sakata la Chadema

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Jenerali John Mbungo

Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini Tanzania (Takukuru), imekamilisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha, inazokikabili Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo amesema na Brigedia Jenerali, John Mbungo, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, wakati anazungumza na MwanaHALISI ONLINE, kwa simu, leo Jumamosi tarehe 27 Juni 2020.

Tarehe 10 Juni 2020, Takukuru ilitangaza kuanza kuwahoji wabunge wa Chadema 69, viongozi waandamizi pamoja na wanachama wa chama hicho, kuhusiana na sakata hilo.

Wanachama hao wa Chadema walihojiwa makao makuu ya taasisi hiyo jijini Dodoma.

Mbungo amesema, kwa sasa Takukuru inachambua maelezo yaliyotolewa na wabunge Chadema, viongozi pamoja na wanachama wa chama hicho, ili kuamua kama kuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha tuhuma hizo.

John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema

“Lakini, taarifa ya uhakika niliyonayo ni sasa hivi wanachambua ushaidi uliopatikana, kwa ajili ya kujua kama ushahidi unatosha ili kusimamisha makosa ya jinai kwa mujibu wa tuhuma ambazo zipo za ubadhirifu wa fedha za wanachama,” amesema Mbungo alijibu swali la MwanaHALISI ONLINE lililotaka kujua kipi kinaendelea juu ya uchunguzi huo

“Kwa sehemu kubwa tumemaliza kuwahoji viongozi waandamizi na viongozi wengine na wanachama, sasa tunachambua taarifa zao na ushahidi ambao wametupa, kuangalia kama utajenga hoja za jinai ili tuweze kufikisha Ofisi ya AG (Mwanasheria Mkuu wa Serikali) kwa jaili ya kuandaa mashtaka,” amesema Mbungo.

Mbungo amesema, miongoni mwa viongozi waandamizi wa Chadema waliohojiwa kuhusiana na sakata hilo ni, kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Vincent Mashinji, aliyekuwa Katibu Mkuu Chadema. John Mnyika, Katibu Mkuu Chadema na mweka hazina wa chama hicho na wabunge wa Chadema.

Sakata hilo lilibuka baada ya wanachama kadhaa wa Chadema waliokuwa wabunge, kutuhumu chama hicho kufanya ubadhirifu wa fedha walizokuwa wanatoa kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za ujenzi wa chama hicho.

Wabunge hao walisema, hawakuwa na shida kuchangia fedha hizo kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho ila matumizi ya fedha hizo ndicho walikuwa wanahoji kwamba hawafahamu zilivyotumika.

Miongoni mwa watu walioibua tuhuma hizo ni, Peter Lijualikali, Mbunge wa Kilombero na David Silinde wa Momba ambao wote wamejiunga na CCM.

Wengine ni, wabunge viti maalumu, Susan Maselle na Joyce Sokombi ambao wamejiunga na NCCR-Mageuzi.

Hata hivyo, mara kadhaa Chadema kupitia kwa viongozi wake, walikanusha tuhuma hizo wakisema kwamba, wakisema, fedha hizo zilikatwa kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho na matumizi yalifanyika sawia na kukagiliwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

error: Content is protected !!