February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Bosi sekretarieti ya maadili afariki, JPM amlilia

Rais John Magufuli

Spread the love

ALIYEKUWA Kamishana wa Sekretarieti ya Maandili ya Viongozi wa Umma nchini Tanzania, Jaji mstaafu Harold Nsekela amefariki dunia. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Taarifa za kifo chake, zimetolewa leo Jumapili tarehe 6 Desemba 2020 na Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli kupitia akaunti yake ya Twitter.

Hata hivyo, Rais Magufuli hajaeleza, Jaji Nsekela amefikwa na mauti kwa tatizo gani au hospitali aliyokuwa amelazwa.

“Nimesikitishwa na kifo cha Kamishna wa Maadili, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Harold Nsekela. Poleni familia, watumishi wote wa Sekretarieti ya Maadili na Mahakama.”

“Jaji mstaafu Nsekela alikuwa mwadilifu, mzalendo, asiyejikweza na mchapakazi. Mungu amweke mahali pema, Amina,” amesema Rais Magufuli

error: Content is protected !!