Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Bosi’ MSD, mwenzake waendelea kusota rumande
Habari Mchanganyiko

Bosi’ MSD, mwenzake waendelea kusota rumande

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu
Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam nchini Tanzania imeleezwa upelelezi wa kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na Kaimu Mkurugenzi wa Lojistiki, Byekwaso Tabura, bado unaendelea. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Bwanakunu na Tabura wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matano likiwemo la kutakatisha fedha kiasi cha Sh.1.6 bilioni.

Hayo yameelezwa leo Jumatatu tarehe 27 Julai 2020 na upande wa mashkata wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutwaja.

Mbele ya hakimu Mkuu, Richard Kabate, wakili wa Takukuru, Moza Kasubi amedai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Kabate baada ya kusikiliza hoja hizo ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 10, 2020 itakapotajwa.

Miongoni mwa mashtaka yanayowakabili washtakiwa ni kati ya tarehe 1 Julai, 2016 na 30 June, 2019 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, kwa makusudi washtakiwa waliongoza genge la uhalifu.

Laurean Bwanakunu, aliyekuwa Mkurugenzi wa MSD

Shtaka la pili ni kuisababishia hasara MSD, tukio wanalodaiwa kulitenda kati ya Julai mosi, 2016 na tarehe 30 June, 2019, katika eneo la MSD lililopo Keko, washtakiwa waliisababishia MSD hasara ya Sh 3.8 bilioni.

Pia, Bwanakunu, anadaiwa kati ya tarehe 1 Julai, 2016 na 30 Juni, 2019 katika Ofisi za MSD zilizopo Keko, kwa makusudi alikiuka sheria ya umma kwa kutumia madaraka yake vibaya kwa kuwaongezea nyongeza ya mishahara na posho wafanyakazi wa MSD, bila kibali cha Katibu Mkuu Utumishi na hivyo kuisababishia hasara Mamlaka hiyo kiasi cha Sh 3bilion.

Shtaka la nne ni kuisababishia hasara ya Sh. 85 milioni mamlaka, shtaka linalowakabili washtakiwa wote, huku katika shtaka lingine wakituhumiwa kutakatisha kiasi cha Sh.1.6 bilioni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari Mchanganyiko

GGML yasisitiza kuendelea kuimarisha afya za wafanyakazi

Spread the loveKAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited kwa kushirikiana na kampuni...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

error: Content is protected !!