BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), inatarajiwa kutoa mikopo kwa wanafunzi 128,285 sawa na ongezeko la asilimia 4.5 ikilinganishwa na mwaka wa fedha uliopita (2018/19). Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Kati yao, wanafunzi 45,485 watakuwa wa mwaka wa kwanza ikiwa ni ongezeko la silimia 10.3 ikilinganishwa na wanafunzi 41,234 wa mwaka 2018/19.
Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 29 Aprili 2019 bungeni na Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia wakati akiwasilisha bungeni Makadilio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2019/2020.
Prof Ndalichako amesema kuwa, bodi hiyo itafuatilia fedha inayolipwa ili kuhakikisha fedha za mikopo zinawafikia kwa wakati wanafunzi stahiki.
Amesema, bodi hiyo imepanga kutekeleza mambo kadhaa ambayo ni kutoa mikopo yenye thamani ya Sh, 450 Bil ambapo ni ongezeko la asilimia 5.0 ikilinganishwa na mwaka 2018/19.
“Kukusanya Sh. 221.5 Bil kutoka kwa wanufaika ambao mikopo yaio imeiva, hili ni ongezeko la asilimia 40.5 ukilinganuisha na lengo la mwaka 2018/19 ambalo ni Sh. 157.7 Bil,” amesema.
Prof. Ndalichako amesema, HESLB itaanzisha na kuimarisha ofisi mbili za kanda katika Mikoa ya Mbeya na Mtwara ili kufikisha jumla ya ofisi sita za kanda.
Leave a comment