January 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Bodi ya Ligi yafungia viwanja saba

Uwanja wa Nangwanda Sijaona wa Mtwara

Spread the love

BODI ya Ligi imevifungia viwanja vya Majimaji (songea), Mkwakwani (Tanga), Sabasaba (Njombe), Ali Hassan Mwinyi (Tabora), Kipija (Mbeya), Nagwanda Sijaona (Mtwara) na Jamhuri (Dodoma) mara baada ya kukosa baadhi ya sifa ili viweze kutumika kwenye michezo ya kimashidano. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa kutoka ndani ya bodi hiyo imeleza kuwa viwanja hivyo vilivyokuwa vinatumika kwa michezo ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza havitatumika kwa sasa mpaka vitapofanyiwa marekebisho na kamati ya leseni kukagua na kujilidhisha.

Sababu kubwa ya kuvifungia viwanja hivyi ni kuwa na maeneo mabovu ya kuchezea (pitch), mabenchi ya kukaa wachezaji wa akiba sambamba na vyumba vya kubadilishia nguo.

Kwa mantiki hiyo klabu zote zilikuwa zinacheza kwenye viwanja hivyo kwa michezo yake ya nyumbani vitalazimika kutafuta viwanja vingine vyenye sifa ili waweze kutumia kwenye michezo yao ya kimashindano.

error: Content is protected !!