Bobi Wine atinga mahakamani na magongo, aachiwa kwa dhamana

ROBERT Kyagulanyi ‘Bob Wine’ Mbunge wa jimbo la Kyadondo nchini Uganda na wabunge wengine watatu wameachiwa huru kwa dhamana na Mahakama Kuu mjini Gulu. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Wabunge hao watatu waliokuwa wakizuiliwa kwa takribani wiki mbili wameachiwa huru leo tarehe 27 Agosti, 2018 pamoja na watuhumiwa wengine nane.

Uamuzi huo wa mahakama umetolewa na Steven Mubiru, Jaji wa Mahakama Kuu.

Kabla ya watuhumiwa hao kuachiwa huru, Atiku Shabani mmoja kati ya watuhumiwa katika kesi hiyo alianguka ghafla wakati kesi hiyo ikisikilizwa katika chumba cha mahakama kuu ya Gulu.

Leo tarehe 27 Agosti, 2018 watuhumiwa wa kesi hiyo walifikishwa mahakamani kwa ajili ya usikilizwaji wa maombi yao ya dhamana.

Kufuatia tukio hilo, Jaji Mubiru aliamuru mtuhumiwa huyo kutolewa nje ya chumba cha mahakama.

ROBERT Kyagulanyi ‘Bob Wine’ Mbunge wa jimbo la Kyadondo nchini Uganda na wabunge wengine watatu wameachiwa huru kwa dhamana na Mahakama Kuu mjini Gulu. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea). Wabunge hao watatu waliokuwa wakizuiliwa kwa takribani wiki mbili wameachiwa huru leo tarehe 27 Agosti, 2018 pamoja na watuhumiwa wengine nane. Uamuzi huo wa mahakama umetolewa na Steven Mubiru, Jaji wa Mahakama Kuu. https://www.youtube.com/watch?v=nhdsYBYwfRg Kabla ya watuhumiwa hao kuachiwa huru, Atiku Shabani mmoja kati ya watuhumiwa katika kesi hiyo alianguka ghafla wakati kesi hiyo ikisikilizwa katika chumba cha mahakama kuu ya Gulu. Leo tarehe 27 Agosti, 2018 watuhumiwa wa kesi hiyo…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Regina Mkonde

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram