Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Biwott kuzikiwa jeneza lisopitisha risasi
Habari za SiasaKimataifa

Biwott kuzikiwa jeneza lisopitisha risasi

Jeneza lililosarifiwa kwa dhahabu na ambalo lina uwezo wa kutopenya risasi atakalozikwa nalo Marehemu Nicolas Biwott.
Spread the love

MWANASIASA mkongwe aliyekuwa na nguvu kubwa nchini Kenya, Nicolas Biwott atazikwa kwa kutumia jeneza lililosarifiwa kwa dhahabu na ambalo lina uwezo wa kutopenya risasi, anaandika Jabir Idrissa.

Kulingana na wosia aliouandika mapema kabla ya kifo chake kilichotokea jijini Nairobi, wiki iliyopita, aliamua kuzikwa kwa utaratibu huo mwenyewe akisema utamwezesha kutofikiwa na maadui zake.

“Hata ukifa maadui zako watakufuata tu kaburini. Nitakapokufa nije kuzikwa ndani ya jeneza lililowekwa kinga ya kupenya risasi ili kuwazuia wenye nia ya kunifikia kunidhuru,” amesema katika wosia wake.

Pia amewaasa ndugu na rafiki zake kumzika kwenye jeneza lililotengenezwa kwa mapambo ya dhahabu ili kuendana na hadhi yake alipokuwa hai.

Jeneza kwa ajili yake limetengenezwa nchini Marekani na linatarajiwa kuwasili siku yoyote wiki hii likiwa linalindwa dhidi ya uharibifu au kuibwa.

                               Marehemu Nicolas Biwott.

Biwott ambaye alifikia ngazi ya uwaziri katika serikali ya kwanza baada ya uhuru wa 1962 ya Jomo Kenyatta na baadae akawa karibu na marais waliofuata Daniel arap Moi na Mwai Kibaki, alikuwa kiongozi ambaye muda wote akihofia kuuawa.

Mtu aliyekuwa msiri sana na tajiri, hakuruhusu hata mara moja mgeni karibu na nyumbani kwake isipokuwa tu kwa ambaye aliridhika hawezi kumdhuru. Ndio maana basi, hata hivi ameaga dunia, amependa ahifadhiwe dhidi ya maadui.

Kwenye mitandao ya kijamii kumechapishwa orodha ndefu ya kampuni ambazo yeye ni mmiliki wa asilimia 100 ya hisa. Baadhi ya kampuni akizimiliki kwa ubia na Moi, aliyeshika urais baada ya mzee Kenyatta, baba wa Rais Uhuru Kenyatta anayewania tena urais baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa mwaka 2012.

Kama ilivyokuwa katika uchaguzi huo, Uhuru anakabiliwa na ushindani mkali mbele ya Raila Odinga, mwanasiasa makini na mwana wa makamo wa rais mzee Kenyatta, mzee Jaramogi Odinga.

Written by
Jabir Idrissa

+255 774 226248

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!