Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Bilioni 13 zinavyoboresha sekta ya elimu Kasulu
Elimu

Bilioni 13 zinavyoboresha sekta ya elimu Kasulu

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akitoa maelekezo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ualimu Kabanga kanachojengwa katika Halmashauri ya Kasulu mkoani Kigoma.
Spread the love

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Profesa Joyce Ndalichako amekagua miradi ya elimu inayotekelezwa katika Halmashauri ya Kasulu mkoani Kigoma yenye thamani ya zaidi ya Sh. 13 bilioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kigoma … (endelea).

Miradi hiyo ni pamoja na  ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Kasulu, Chuo cha Ualimu Kabanga na jengo la Utawala la shule ya Sekondari Grand.

Profesa Ndalichako, amefanya ukaguzi huo jana Jumanne tarehe 30 Juni 2020.

Akizungumzia maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ualimu Kabanga, Profesa Ndalichako alisema, kinajengewa upya miundombinu yote baada ya ile ya awali kuchakaa na kushindwa kukarabatiwa.

Alisema ujenzi wa miundombinu ya chuo  hicho unagharimu zaidi ya Sh. 10 bilioni na utakapokamilika utabadili taswira ya mji huo kwa kuwa majengo yanayojengwa ni ya kisasa na imara ambayo yatadumu kwa muda mrefu.

Muonekano wa jengo jipya la utawala la shule ya sekondari Granda lililojengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia likiwa katika hatua za mwisho za ukamilishwaji

Kuhusu ujenzi wa jengo jipya la utawala na utengenezaji wa mfumo wa maji katika shule ya sekondari ya Grand, Profesa Ndalichako alisema, umegharimu zaidi ya Sh. 534 milioni na kwamba utakapokamilika utaongeza morali ya walimu kufundisha na kusaidia wanafunzi waliopo katika shule hiyo.

Mradi mwingine uliotembelewa ni ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha wilaya ya Kasulu ambao upo katika hatua za mwisho ukiwa umegharimu zaidi ya Sh. 2.97 bilioni.

Alisema majengo 15 yatajengwa na kitachukua wanafunzi 320 watakaokuwa wakilala chuoni hapo.

Profesa Ndalicahko aliwataka wananchi wa wilaya ya Kasulu na mkoa wa Kigoma kwa ujumla kutumia fursa ya kuwepo kwa vyuo mbalimbali katika Halmashauri hiyo kujipatia maarifa na ujuzi utakaowawezesha kuajiriwa ama kujiajiri ili kujiletea maendeleo binafsi na ya mkoa wa Kigoma.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Simon Anange aliishukuru  Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa namna ilivyojikita katika kupanua wigo wa elimu.

Mhandisi Faraja Magania kutoka Chuo cha Ufundi Arusha akifafanua jambo wakati Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako alipofanya ziara ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Chuo cha Ufundi Kasulu.

Alisema katika wilaya yake, kuna maeneo ambayo ni ya wafugaji na watoto hawakuwa wakienda shule lakini kwa sasa zimejengwa shule shikizi katika maeneo hayo ya mbali hivyo kuwezesha watoto kusoma na kuleta matokeo chanya.

Kanali Anange alisema baada ya Serikali kutekeleza Sera ya Elimu bila ada, kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi, hivyo kusababisha Serikali kupanua miundombinu katika ngazi zote za elimu ili kuwezesha fursa za masomo kwa wanafunzi ikiwemo kuongeza walimu.

Alisema ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika sekta ya elimu itawezesha vijana wa Kitanzania kupata elimu katika mazingira bora.

Naye Mratibu wa Mradi wa Uendelezaji wa Elimu ya Ualimu (TESP), Ignas Chonya alisema ujenzi wa miundombinu katika Chuo cha Ualimu Kabanga awamu ya kwanza unatarajiwa kukamilika Oktoba 2020, chuo kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanachuo 400 kwa wakati mmoja na kwamba chuo kinatarajiwa kuanza mafunzo mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

error: Content is protected !!