Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Bil. 1.7 zakosa mkopaji Dodoma
Habari Mchanganyiko

Bil. 1.7 zakosa mkopaji Dodoma

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi
Spread the love

MKURUGENZI wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi amewataka vijana, akina mama na watu wenye ulemavu kuanzisha vikundi na kuweza kupatiwa mikopo kwa ajili ya maendeleo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kunambi alisema kuwa mpaka sasa katika mfuko wa kuwakopesha vijana, akina mama na watu wenye ulemavu una fedha kiasi cha zaidi ya bilioni 1.7 lakini hakuna vikundi ambavyo vinajitokeza kukopa fedha hizo.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa vijana wengi wamekuwa wakitumia muda mwingi kukaa vijiweni bila kuwa na shughuli yoyote ya uzalishaji na badala yake wanalalamika kwa madai kuwa maisha ni magumu.

Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi huyo, alisema kuwa kutokana na jiji kuwa na mapato makubwa kwa hivi sasa kuna fedha za kutosha ambazo vijana,akina mama na watu wenye ulemavu wanaweza kujiunga nakupatiwa mikopo.

“Nataka kuwaambia vijana, akina mama na watu wenye ulemavu waanzishe vikundi na waweze kuomba mkopo kwa ajili ya kujiendeleza kwani pesa hipo ya kutosha lakini cha kushangaza walengwa hawataki kuchangamkia fursa.

“Kwa sasa hakuna haja ya vijana na makundi mengine kukaa vijiweni wanalalamika kuwa maisha ni magumu wakati kuna fursa za kutosha katika jiji la Dodoma kwa sasa kuna fedha zaidi ya Sh. 1.7 bilioni na hizo hazina wakopaji makundi ambayo yanastahili wala hayafanyi kazi yoyote ya kujiendeleza,” alisema Kunambi.

Katika hatua nyingine Kunambi aliwataka vijana kuachana na tabia ya kulalamika bila kufanya kazi na badala yake watumie fursa zinazopatikana katika jiji la Dodoma kutokana na shughuli mbalimbali za ujenzi zinazoendelea.

Alisema kuwa kwa sasa jiji la Dodoma lina shughuli nyingi ikiwemo shughuli ya ujenzi wa mji wa kiserikali, ujenzi wa sendi kuu ya mabasi pamoja na ujenzi wa treini ya mwendo kasi.

“Unaweza kutumia nguvu yako kufanya kazi kwa kujipatia kipato lakini kama unaujuzi unaweza kutumia ujuzi wako kwa ajili ya kujiongezea kipato kwani siamini kama ukiamka asubuhi ukaanza kuzungukia kwenye site zinazoendelea kujengwa kama utakosa kazi ya kufanya.

“Kwa sasa mkoa wa Dodoma unafursa nyingi kutokana na shughuli zinazofanyika kwa maana ya maadalizi ya wafanyakazi wote na wizara zote kuhamia Dodoma, ndiyo maana nawasisitiza hata vijana, akina mama na watu wenye ulemavu kujiunga kwenye vikundi ili waweze kupata mkopo kwani fursa ni nyingi.

“Akina mama wakijiunga vikundi wanaweza kuanzisha mradi wa kuwapikia chakula mafundi katika site zao za kazi pia wanaweza kusambaza vinywaji na huduma nyingine nying kwa maana nyingine hapo ndipo tunapotumia msemo wa kuwa mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe,” alisema Kunambi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!