February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Bibi amuunguza kwa moto mjukuu wake

Emmanuel Lukula, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro

Spread the love

DARIA Frank (55), Mkazi wa Mamba, Vunjo Mashariki katika Wilaya ya Moshi, Kilimanjaro anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuunguza kwa moto mjukuu wake. Anaripoti mwandishi wetu, Kilimanjaro…(endelea).

Mjukuu huyo ni mwanafunzi wa darasa la awali katika Shule ya St. Paul Albert. Jeshi la Polisi Moshi limeeleza, mtoto huyo amesababishiwa maumivu makali.

Akizungunza na vyombo vya habari  leo tarehe 17 Julai 2020, Emmanuel Lukula, Kamanda wa Polisi mkoani humo amesema, mtoto huyo alifanyiwa kitendo hicho na bibi yake mzaa baba tarehe 10 Julai 2020 katika eneo la Mamba saa 5:00 asubuhi.

Kamanda Lukula amesema, mtoto huyo ameunguzwa kwenye sehemu mbalimbali za mwili kuanzia chini ya kiuno hadi magotini. Kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi.

Jeshi hilo limeeleza kwamba linaendeleo na uchunguzi wa tukuio hilo ili kubaini chanzo chake.

”Jeshi la Polisi tunamshikilia mwanamke huyu kwa mahoniano zaidi, ili kubaini chanzo cha tukio hili la kinyama na la kikatili,” amesema na kuongeza:

“Mtoto huyo ana umri wa miaka sita, aliunguzwa na moto kuanzia chini ya kitovu hadi miguuni, wakati mtoto huyo akiendelea kuungua na moto, majirani walisikia kelele za vilio kutoka kwa mtoto huyo ndipo walipofika nyumba ka bibi huyo kwa ajili ya   kutoa msaada.”

error: Content is protected !!