July 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Biashara kuipa ubingwa Simba kama Chelsea dhidi ya Liverpool?

Spread the love

HUWENDA ubingwa wa Simba ukaamuliwa na Biashara United, kama ilivyokuwa kwa Liverpool kuamuliwa ubingwa na Chelsea baada ya kumfunga Manchester City kwa mabao 2-1. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam… endelea

Liverpool ilitangaza ubingwa juzi wakiwa nyumbani na huwenda hali hiyo ikajitokleza leo Jumamosi tarehe 27 Juni 2020 kwa Simba kutangaza ubingwa wakiwa Hotelini, jijini Mbeya kwa kusubiri matokeo ya mchezo kati ya Biashara United dhidi ya Azam FC utakaopigwa kwenye Uwanja wa Karume mkoani Mara.

Kwenye mchezo huo wa leo, kama Biashara United itafanikiwa kuifunga Azam FC, basi klabu ya Simba itatangazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye msimu wa 2019/20.

Simba huwenda ikatangaza ubingwa ikiwa imesalia michezo saba na pointi 78, kama ilivyokuwa kwa Liverpool kwa kutangaza ubingwa huku ikiwa imebaki michezo saba na kukusanya pointi 86.

Mpaka sasa Azam FC inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 58 na kama ikifanikiwa kushinda kwenye mchezo wa leo, basi itawalazimu Simba kusubiri ushindi kwenye mchezo wa kesho Jumapili dhidi ya Tanzania Prisons, utakaochezwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Jijini Mbeya.

Na kama Simba itafanikiwa kushinda kesho na kutangza ubingwa basi itakuwa inashikilia taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo toka msimu wa 2017/18.

Ukiacha mchezo huo Ligi hiyo pia itaendelea leo kwa kupigwa michezo mingine Saba ambapo Yanga ataikaribisha Ndanda kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam, Ruvu Shooting dhidi ya Namungo, Alliance kuikabili Coastal Union, Mwadui watakuwa nyumbani kuwakalibisha Mtibwa Sugar, Mbeya City dhidi ya Jkt Tanzania.

Singida United watakuwa Namfua kujiuliza mbele ya Lipuli Fc na mchezo wa mwisho utapigwa kwenye dimba la Kaitaba, Kagera kwa kuwakutanisha wenyeji Kagera Sugar dhidi ya KMC.

error: Content is protected !!