July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Benki ya TPB, TIB Corparate zaunganishwa

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imetangaza kuziunganisha Benki ya TPB na TIB Corparate kuanzia leo tarehe 1 Juni, 2020. Anaripoti Mwandishi, Dodoma … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Jumatatu tarehe 1 Juni, 2020, Msajili wa Hazina nchini Tanzania, Athuman Mbutuka amesema, madeni na mali zote za TIB zitachukuliwa na TPB.

Amesema lengo la kuziunganisha taasisi hizo ni kuongeza ufanisi na kupunguza gharama, “ili kuwa na benki moja imara ya biashara. Muungano huu, utaleta mageuzi mkaubwa ya kiutendaji, muundo na taswira kwa ujumla ili iweze kushindana.”

“Kwa hatua hii tuliyofikia, Benki ya TPB inachukua mali na madeni yote ya iliyokuwa benki ya TIB Corparate na uamuzi huu, umeridhiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT),” amesema Mbutuka

Amesema, Serikali itaendelea kusimamia utendaji wa benki zote ili  ziimarike kwa maslahi ya wateja.

error: Content is protected !!