Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Benki ya Dunia yaipa kibano kingine serikali ya Magufuli
Habari za SiasaTangulizi

Benki ya Dunia yaipa kibano kingine serikali ya Magufuli

Rais John Magufuli
Spread the love
BENKI ya Dunia (WB), yaweza kuhamisha ofisi yake ya Mkurugenzi Mkazi kutoka jijini Dar es Salaam na kuipeleka nchini Afrika Kusini. Anaandika Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa kutoka Washinton DC, Marekani, Dar es Salaam na Dodoma zinasema, uamuzi wa benki hiyo kuhamishia ofisi yake ya Mkurugenzi Mkazi nchini Afrika Kusini, umetokana na kinachoitwa, “kuzorota kwa mahusiano kati ya benki hiyo na serikali ya Tanzania.”

Mbali na kufunga ofisi yake ya mkurugenzi mkazi, mtoa taarifa wetu anasema, benki hiyo bado inaendelea na msimamo wake wa kuzuia mabilioni ya shilingi iliyoyatoa kwa kwa serikali, hadi hapo mahusiano hayo yatakaporejea kwenye hali ya kawaida.

Kuzorota kwa mahusiano kati ya Tanzania na benki hiyo, kunatokana na hatua ya serikali kupitisha sheria ya Takwimu ya mwaka 2018. Sheria ya Takwimu ilipitishwa katika mkutano wa Bunge wa Septemba mwaka jana. 

Benki ya dunia imetenga takribani dola za Kimarekani 1.7 bilioni (karibu Sh. 4.1 trilioni), kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo, lakini mabilioni hayo ya shilingi yamezuiliwa kutokana na kupitishwa kwa sheria hiyo. 

“Ni kweli kwamba benki yetu (WB), imepanga kuhamisha ofisi ya Mkurugenzi Mkazi wa kutoka Dar es Salaam nchini Tanzania kwenda Afrika Kusini,” ameeleza afisa mmoja wa ngazi ya juu wa benki hiyo aliyepo nchini Marekani.

Amesema, “jambo hili tumelieleza vizuri kwenye mazungumzo yetu na ujumbe wa serikali ya Tanzania ulipokuja hapa Washington DC, mwezi uliyopita. Benki imesema, haitatoa fedha zake za miradi ya maendeleo, hadi hapo sheria hiyo ya takwimu itakapofanyiwa marekebisho.”

Ujumbe wa serikali ya Tanzania uliokwenda nchini Marekani, ulifanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa benki hiyo, anayeshughulikia masuala ya Afrika, Hafez Ghanem na Mkurugenzi Mtendaji wa benki anayesimamia nchi za Afrika, Anne Kabagambe.

Fedha ambazo benki ya dunia imeziondoa, ni pamoja na dola za Marekani 450 milioni, zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya kusaidia miradi ya TASAF 111 na dola za Kimarekani 300 milioni, zilizotengwa kwa ajili ya kusambaza maji safi vijijini.

Fedha nyingine, ni zile zilizotengwa kwa ajili ya kuongeza ubora wa elimu ya sekondari. Katika mradi huo, WB ilikuwa imetenga kiasi cha dola za Marekani 400 milioni.

Benki ya dunia na shirika la fedha la kimataifa (IMF), zimeungana na baadhi ya wadau nchini, kudai kufanyiwa marekebisho sheria hiyo kwa maelezo kuwa inakiuka haki za binadamu na kuminya uhuru wa wananchi wa kujieleza na wa kutoa maoni.

Baadhi ya vifungu vinavyolalamikiwa, ni pamoja na kifungu cha 24 (A) (2); 24 (B) (1) pamoja na 24 (B) (2).

Tangu kufanyiwa mabadiliko sheria ya takwimu nchini, watu kadhaa, wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuchapisha taarifa kinyume na sheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!