Bei ya vyakula yapaa Morogoro

WAKAZI wa Mji wa Morogoro wamelalamika kupanda maradufu kwa bei ya vyakula ikiwemo magimbi, mihogo, viazi pamoja na sukari, anaandika Christina Haule.

Mwandishi wa Mwanahalisi Online ameshuhudia hali hiyo kwenye maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Morogoro.

Katika soko kuu la manispaa hiyo pamoja na soko la matunda la Mawenzi hali ni hiyo hiyo ambapo wateja wamelazimika kununua magimbi kwa bei ya shilingi 3,000 badala ya 1,000 bei ya awali.

Akizungumzia hilo Aqram Muhamedi, mkazi wa manispaa hiyo amesema kuwa, wanashangazwa na wafanyabiashara hao kutumia vibaya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa kupandisha bidhaa kiholela.

James Kimambo, mfanyabiashara wa duka sokoni hapo amesema kuwa, wamelazimika kuuza sukari kwa bei ya juu (3600) kwa wateja wao kutokana na namna wanavyoinunua.

 

WAKAZI wa Mji wa Morogoro wamelalamika kupanda maradufu kwa bei ya vyakula ikiwemo magimbi, mihogo, viazi pamoja na sukari, anaandika Christina Haule. Mwandishi wa Mwanahalisi Online ameshuhudia hali hiyo kwenye maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Morogoro. Katika soko kuu la manispaa hiyo pamoja na soko la matunda la Mawenzi hali ni hiyo hiyo ambapo wateja wamelazimika kununua magimbi kwa bei ya shilingi 3,000 badala ya 1,000 bei ya awali. Akizungumzia hilo Aqram Muhamedi, mkazi wa manispaa hiyo amesema kuwa, wanashangazwa na wafanyabiashara hao kutumia vibaya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa kupandisha bidhaa kiholela. James Kimambo, mfanyabiashara wa duka sokoni hapo amesema…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Hamisi Mguta

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube