Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bawacha wawananga Mdee na wenzake
Habari za Siasa

Bawacha wawananga Mdee na wenzake

Spread the love

BARAZA la Wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha) limesema, kuondoka kwa mwenyekiti wake, Halima Mdee na wenzake 18, hawatarudisha nyuma jitihada za wanawake kupigania demokrasia. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa na baadhi ya wenyeviti wa Bawacha wa mikoa wakati wakizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Chadema Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Jumamosi tarehe 28 Novemba 2020.

Wenyeviti hao, walikuwa wakitoa mrejesho wa kikao cha kamati tendaji ya Bawacha ikiwa ni siku moja imepita tangu kamati kuu ya Chadema ilipotangaza kuwafuta uanachama Mdee na wenzake 18 kwa tuhuma za usaliti.

Nafasi za juu za uongozi wa Bawacha, aliyebaki ni Makamu Mwenyekiti Zanzibar- Sharifa Suleiman Khamis huku Mwenyekiti, makamu mwenyekiti Bara, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu Bara na Zanzibar na Katibu Mwenezi Mwenezi akiwawa miongoni mwa waliofukuzwa.

Sharifa amesema, nafasi zilizowazi zitajazwa hivi karibuni.

Mbali na kutangaza ujazwaji wa nafasi hizo, Khamis amewaagiza viongozi wa Bawacha katika mikoa kuendelea na shughuli za ujenzi wa baraza hilo na Chadema.

“Kutoka hivi sasa, wanawake wote turudi majimboni kwetu kuendelea kufanya ujenzi wa chama, kama ujenzi wa chama unavyokwenda.”

“Naunga mkono uamuzi wa kamati kuu wa kuwavua uanachama wezetu 19, Kuanzia sasa, tutaendelea kujenga chama na kuondoka kwao si kitu wala chochote. Mdee alipata heshima kupitia Chadema lakini sasa haeleweki,” amesema Sharifa

Naye aliyekuwa mbunge wa Mlimba, Susan Kiwanga amesema, “jana kamati kuu umemchinja ng’ombe vile vile alivyolala. Bawacha iko imara na tutaendelea kupigania haki, wanawake tuko imara sana na kuondoka kwao hakutaturudisha nyuma.”

Kwa upande wake, mwekahazina wa Bawacha, Catherine Ruge amesema “viongozi wetu wakuu wa Bawacha kukisaliti chama. Halima Mdee tulimwamini na kumwona kama kiongozi shupavu na jasiri, lakini 24 Novemba 2020 aliamua kubadili historia yake.”

“Tunaipongeza sana kamati kuu chini ya Freeman Mbowe kwa uamuzi walioufanya. Sisi wanawake wa Chadema, tutakilinda chama hiki kwa wivu mkubwa,” amesema Catherine ambaye alikuwa mbunge wa viti maalum.

 

Wabunge wengine waliofukuzwa ni wale waliokuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Ester Bulaya na Esther Matiko. Katibu Mkuu wa Bavicha, Nusrat Hanje. Katibu Mkuu Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Grace Tendega.

Makamu Mwenyekiti Bawacha (Bara), Hawa Mwaifunga. Naibu Katibu Mkuu Bawacha, Jesca Kishoa na Katibu Mwenezi Bawacha, Agnesta Lambat.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa Mtwara, Tunza Malapo, Ceciia Pareso, Asia Mwadin Mohamed, Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Siyao.Salome Makamba, Anatropia Theonest na Conchesta Lwamlaza.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!