Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bawacha wanunua kesi ya mwanamke kujifungua Polisi
Habari za Siasa

Bawacha wanunua kesi ya mwanamke kujifungua Polisi

Katibu Mkuu wa Bawacha, Grace Tendega
Spread the love

UONGOZI wa Baraza la wanawake Chadema (Bawacha)limelaani vikali kitedendo cha udhalilishaji kilichofanywa na jeshi la polisi dhidi ya Amina Mapunda (26) mkazi wa Kiswanya kijiji cha Mgundeni, tarafa ya Mang’ula wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Uongozi huo ulisema kuwa kitendo cha mwanamke huyo kujifungulia nje ya kituo cha polisi bila msaada wowote ni kitendo cha kinyama na kinatoa picha ni kwa jinsi gani jeshi la polisi linafanya kazi yake bila ueledi wa kutosha.

Akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Bawacha, Grace Tendega na mbunge wa Viti maalumu amesema viongozi huo unalaani kitendo hicho na viongozi ndani ya jeshi la polisi wanatakiwa kujipima na kujitafakari kama kweli wanatosha au wajiuzulu.

Amesema kitendo cha jeshi hilo kumsababishia mwanamke huyo kujifungulia chini tena kwenye mchanga hakimdhalilishi yeye peke yake bali kinawadhalilisha akina mama wengi wa kitanzania na niukiukwaji wa haki za binadamu.

“Hapa unaweza kujiuliza mama anahusikaje na wizi wa mume wake,haya kama kweli waliona kuna vifaa vya wizi kwanini hawakuchukua vifaa hivyo kama ushahidi.

“Lakini inashangaza hao polisi hawakuona kama huyo mama ni mjamzito au hawajui mtu ambaye ni mjamzito,haya ni mambo ya ajabu sana kwa jeshi la polisi,” amesema Tendega.

Katika hatua nyingine Tendega amesema kama kweli jeshi la polisi lingekuwa na ueledi wa kazi yao ni kwanini wasingeweka matangazo kila kona kwa ajili ya kumsaka mharifu hadi wampate.

Katibu huyo mkuu wa Bawacha amesema kitendo hicho ni kibaya na kuna kila sababu ya viongozi wa Jeshi la Polisi kuanzia ngazi ya Mkuu wa polisi wilaya ya Kilombero, mkuu wa polisi Mkoa wa Morogoro, Mkuu wa Jeshi la polisi Tanzania (IGP) pamoja na Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi na Naibu wake wakajitafakari na kujipima kama kweli wanastahili kuendelea na kazi.

Amesema matukio ya aina hiyo yamekuwa yanajirudia mara kwa mara na jeshi la polisi limekuwa likikaa bila kuonesha juhudi yoyote ya kuwachukulia hatua wanaohusika na uharifu wa kuwatesa wananchi au kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji.

Tendega amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa vitisho mbalimbali lakini chama hicho na Baraza la Wanawake wa Chadema hawatanyamaza na badala yake kitapaza sauti kwa ajili ya kuwatetea wanyonge na kudai haki bila kuwa na woga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!