Patrick Ole Sosopi, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) akiwa jukwaani

BAVICHA kumuombea Tundu Lissu

IKIWA ni wiki moja tangu kupigwa risasi za moto mbunge wa  Singida Mashariki Tundu Lissu Chadema), Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), linatarajia kufanya maombi maalumu ya kitaifa, anaandika Faki Sosi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo makamu  mwenyekiti wa BAVICHA,   Patrick Ole Sosopi amesema  maombi hayo yatajumuisha madhehebu ya dini zote na yatafanyika jumapili ijayo Septemba  17 , mwaka huu.

Amesema maombi hayo yatafanyika katika viwanja vya TP Sinza darajani jijini Dar es Salaam na kuwa hatarajii Jeshi la Polisi kuzuia maombi hayo na badala yake kufika kwa ajili ya kuimarisha ulinzi.

Hata hivyo, ameeleza kuwa tayari jeshi hilo wameshalipelekea taarifa ya kutekelezwa kwa maombi hayo.

IKIWA ni wiki moja tangu kupigwa risasi za moto mbunge wa  Singida Mashariki Tundu Lissu Chadema), Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), linatarajia kufanya maombi maalumu ya kitaifa, anaandika Faki Sosi. Akizungumza na waandishi wa habari leo makamu  mwenyekiti wa BAVICHA,   Patrick Ole Sosopi amesema  maombi hayo yatajumuisha madhehebu ya dini zote na yatafanyika jumapili ijayo Septemba  17 , mwaka huu. Amesema maombi hayo yatafanyika katika viwanja vya TP Sinza darajani jijini Dar es Salaam na kuwa hatarajii Jeshi la Polisi kuzuia maombi hayo na badala yake kufika kwa ajili ya kuimarisha ulinzi. Hata hivyo, ameeleza kuwa…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Faki Sosi

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube