Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Basi la Abood lapata ajali, dereva anusurika kifo
Habari Mchanganyiko

Basi la Abood lapata ajali, dereva anusurika kifo

Spread the love

DEREVA wa basi  la Abood lenye namba za usajili T 269 DBV ambaye jina lake halikufahamika mara moja amenusurika kifo baada ya kushambuliwa na wananchi wenye hasira, baada ya kugonga pikipiki aina ya Boxer. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Ajali hiyo imetokea maeneo ya Mbezi Kwa Msuguri baada ya gari hilo lililokuwa linafukuzana na basi lingine la BM katika barabara mpya na kuigonga pikipiki iliyokuwa inayokea njia ya pembeni na kuingia barabara kubwa.

Baada ya tukio hilo, dereva wa Abood alishuka kwa lengo la kuangalia kilichotokea, ndipo wananchi walipomvamia na kuanza kumshambulia, kabla ya kufanikiwa kukimbia na kurudi kwenye gari na kufunga milango.

Hali hiyo ilisababisha usumbufu kwa abiria ambao walikuwa wakitaharuki na kulazimika kutokea madirishani mpaka hapo walipofika polisi na kumuamuru dereva kufungua milango la kutoka nje.

Hakuna aliyefariki katika ajali hiyo, lakini mwanamke mmoja ambaye alikuwa abiria wa bodaboda (jina lake halikufahamika) alijeruhiwa kwenye mguu, kichwani na mkononi na amekimbizwa katika hospitali ya Bochi iliyopo Mbezi kwa Msuguri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!