Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Bashe awaonya waliowekeza kwenye ushirika
Habari Mchanganyiko

Bashe awaonya waliowekeza kwenye ushirika

Waziri wa Kilimo Tanzania, Hussein Bashe
Spread the love

NAIBU Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Hussein Bashe amepiga marufuku watu waliowekeza kwenye mashamba na majengo ya ushirika kuacha tabia ya kukopea mali za ushirika bila ridhaa ya wanaushirika na Tume ya Ushirika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Bashe ameyasema hayo leo Jumatano tarehe 1 Julai, 2020  wakati alipofanya ziara ya kukagua mashamba makubwa ya wakulima wa mazao mbalimbali ya mahindi na ngano pamoja na kuzungumza na vyama vya ushirika mkoani Kilimanjaro.

Aidha amesema, kumekuwepo na migogoro mbalimbali ya baadhi ya wawekezaji waliowekeza katika mashamba na majengo ya wakulima kukopea mali za wanaushirika hali ambayo imepelekea Serikali kuanza kuhangaika kukomboa mali hizo.

“Ni marufuku kwa nchi nzima hati ya chama cha ushirika mtu yeyote aliyewekeza kwenye shamba la ushirika au jengo la ushirika haruhusiwi kwenda kukopea mali ya ushirika bila ridhaa ya wanaushirika na Tume ya ushirika, kwa sababu tuna kesi nyingi za mali za ushirika zimekopewa, sasahivi Serikali tunahangaika kuzikomboa,” amesema Bashe.

Shamba la ngano

Hata hivyo, amemwagiza mrajisi wa vyama vya ushirika, Dk. Benson Ndyege kuhakikisha anapitia mikataba yote ya wawekezaji waliopo katika mashamba mbalimbali ya vyama vya ushirika wilayani Hai ili kujua utaratibu wa kuwaweka wawekezaji kama ulifatwa.

1 Comment

  • Mheshimiwa Bashe

    Na lile jengo kuuuubwa la Ushirika pale Lumumba linamilikiwa na nani? Na wakulima washirika au na wajanja wachache waliopokonya mali ya wakulima? Tunaomba maelezo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari Mchanganyiko

DC ampongeza Dk. Rose Rwakatare kwa kusaidia waathirika wa mafuriko Mlimba

Spread the loveMWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk.  Rose Rwakatare...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!