Thursday , 18 April 2024
Habari za Siasa

Bashe apongezwa

Innocent Bashungwa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Spread the love

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amempongeza Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwa kiteuliwa kushika nafasi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Bashe aliteuliwa na Rais John Magufuli tarehe 21 Julai 2019, akichukua nafasi ya Bashungwa ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

Akizungunza na Waandshi wa Habari leo tarehe 23 Julai 2019 jijini Dar es Salaam, Bashungwa amesema, Rais Magufuli amefanya uteuzi sahihi kwa kuwaweka yeye na Bashe katika nafasi zinazotegemeana kwa majukumu.

Amesema, Watanzania wategemee makubwa kupitia ushirikiano baina ya wizara hizo mbili.

“Nitumie nafasi hii kumpongeza Hussein Bashe kwa kuaminiwa na rais, ameenda Wizara ya Kilimo kujazia nafasi yangu na katika kikao ambacho nimekutana na watu wa Holland, Waziri alimtuma Bashe kuwakilisha katika kikao hicho, Wizara ya Kilimo na Wizara ya Biashara Rais ametupanga vizuri,” amesema.

Katika hatua nyingine, Bashungwa amezungumzia mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).

Amesema, unatajiwa kufanyika Agosti mwaka huu, na kwamba jitihada za Rais Magufuli za kuiongoza Tanzania kuwa ya viwanda, ndio zimechangia kufuatia Tanzania kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo.

“Tanzania ni sehemu ya SADC lakini upekee wetu ni kwamba sisi ni nchi ina amani, imejaliwa rasilimali na bandari. Ni fursa kwetu ukilinganisha na nchi zingine za SADC, fursa hii ni kubwa na tuitumie,” amesema.

Mkutano huo wa SADC utakaofanyika Agosti mwaka huu, utajumuisha mataifa 16 yanayounda jumuiya hiyo huku Rais Magufuli akichukua kiti cha Uenyekiti kutoka kwa Rais wa Namibia, Hage Geingog. Mkutano wa SADC mara ya mwisho nicni Tanzania ulifanyika mwaka 2003/2004 ambapo rais wa wakati huo, Benjamin Mkapa alichaguliwa kuwa mwenyekiti.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!