Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Baraza la Mawaziri la Dk. Mwinyi hili hapa
Habari za Siasa

Baraza la Mawaziri la Dk. Mwinyi hili hapa

Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar
Spread the love

DAKTARI Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar ametangaza Baraza la Mawaziri huku wizara mbili na nafasi ya manaibu waziri akiziweka kiporo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Akitangaza baraza lake leo tarehe 19 Novemba 2020, Rais Mwinyi amesema, katika wizara zake 15, wizara mbili ameziacha wazi akisubiri iwapo Chama cha ACT-Wazalendo kitaridhia kuunda Serikali ya Umoja wa Kimataifa (SUK) visiwani humo.

Yafuatayo ni majina ya mawaziri na wizara zao.

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI ZANZIBAR:

1. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji – Mheshimiwa Mudrik Ramadhan Soraga.

2. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) – Mheshimiwa Masoud Ali Mohammed.

3. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba na Utawala Bora – Mheshimiwa Haroun Ali Suleiman.

4. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango – Mheshimiwa Jamal Kassim Ali.

5. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi – Mheshimiwa Dokta Khalid Mohammed Salum.

6. Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji na Mifugo – Mheshimiwa Soud Nahoda Hassan.

7. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali – Mheshimiwa Simai Mohammed Said

8. Wizara ya Habari, Vijana na Utamaduni – Mheshimiwa Tabia Mwita Maulid.

9. Wizara ya Biashara ya Maendeleo ya Viwanda. Hakuna Waziri.

10. Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi – Mheshimiwa Riziki Pembe Juma.

11. Wizara ya Maji na Nishati – Mheshimiwa Suleiman Masoud Makame.

12. Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto. Hakuna Waziri.

13. Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale – Mheshimiwa Lela Mohammed Mussa.

14. Wizara ya Uchumi wa Bluu na Uvuvi – Mheshimiwa Abdallah Hussein Kombo.

15. Wizara ya Ujenzi – Mheshimiwa Rahma Kassim Ali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

error: Content is protected !!