BAKWATA yatikiswa bungeni

Spread the love

MBUNGE wa Ubungo (CHADEMA), Saed Kubenea, amehoji hatua ya serikali ya kulipa mamlaka ya mwisho ya kupeleka mahujaji nchini Saudia, Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza bungeni mara baada ya kumalizika kipindi cha maswali na majibu leo Jumatatu, tarehe 7 Mei, Kubenea amesema, “serikali imetoa mamlaka ya mwisho ya kupeleka mahujaji nchini Saudia Bakwata ili kutimiza nguzo kuu ya uislamu.”

Amesema, “jambo hili ni kinyume na Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Hatua hii, ni kinyume na sheria za nchi na kinyume na matakwa ya uislamu na waislamu.

“Hivyo basi, kwa kuwa Bunge ndio chombo kikuu cha wananchi kwa mujibu wa Katiba; chombo hiki kwa mujibu wa Katiba, ndicho kinachosimamia serikali na kuishauri kwa niaba ya wananchi, naomba serikali itueleze kwa nini imetoa mamlaka haya kwa BAKWATA, wakati chombo hiki siyo mali ya waislamu wote?”

Akizungumza kwa hisia kali, Kubenea alisema, “Katiba ya Jamhuri ya Muungano, inatamka kuwa serikali haina dini. Lakini serikali hii, imejiingiza kwenye mambo ya dini na kutaka waislamu wote kwenda Hijja kupitia Bakwata.”

Amesema, “taifa hili lina taasisi 11 zenye usajili sawa kama Bakwata. Kuwalazimisha waislamu wote kutumia Bakwata kwenye mambo ya Hijja, ni kinyume na katiba. Haikubariki.”

MBUNGE wa Ubungo (CHADEMA), Saed Kubenea, amehoji hatua ya serikali ya kulipa mamlaka ya mwisho ya kupeleka mahujaji nchini Saudia, Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Akizungumza bungeni mara baada ya kumalizika kipindi cha maswali na majibu leo Jumatatu, tarehe 7 Mei, Kubenea amesema, “serikali imetoa mamlaka ya mwisho ya kupeleka mahujaji nchini Saudia Bakwata ili kutimiza nguzo kuu ya uislamu.” Amesema, “jambo hili ni kinyume na Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Hatua hii, ni kinyume na sheria za nchi na kinyume na matakwa ya uislamu na waislamu. “Hivyo basi, kwa…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!