Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir

Bakwata watangaza tarehe ya Sikukuu ya Eid

Spread the love

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza kwamba Sikukuu ya Idd El-Adh’haa itakuwa siku ya Juamatatu ya tarehe 12 Agosti, 2019. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 2 Agosti 2019 na Nuhu Mruma, Katibu Mkuu BAKWATA, inaeleza kwamba swala ya Eid itaswaliwa katika Viwanja vya Masjid Kibadeni, Chanika Zogowali wilayani Ilala Jiji la Dar es Salaam.

Pia, taarifa hiyo imesema Baraza la Eid litafanyika viwanjani hapo mara baada ya swala ya Eid.

“Mheshimiwa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir anapenda kuchukua fursa hii kuutangazia umma kuwa Sikukuu itakuwa siku ya Juamatatu tarehe 12 Agosti 2019,” inaeleza taarifa ya Mruma.

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza kwamba Sikukuu ya Idd El-Adh'haa itakuwa siku ya Juamatatu ya tarehe 12 Agosti, 2019. Anaripoti Mwandishi Wetu ... (endelea). Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 2 Agosti 2019 na Nuhu Mruma, Katibu Mkuu BAKWATA, inaeleza kwamba swala ya Eid itaswaliwa katika Viwanja vya Masjid Kibadeni, Chanika Zogowali wilayani Ilala Jiji la Dar es Salaam. Pia, taarifa hiyo imesema Baraza la Eid litafanyika viwanjani hapo mara baada ya swala ya Eid. "Mheshimiwa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir anapenda kuchukua fursa hii kuutangazia umma kuwa Sikukuu itakuwa siku ya Juamatatu tarehe…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!