Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Baada ya viboko; RC Chalamila ‘afunga’ shule
ElimuHabari MchanganyikoTangulizi

Baada ya viboko; RC Chalamila ‘afunga’ shule

Spread the love

ALBERT Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amewarudisha nyumbani wanafunzi wa kidato cha tano na sita wa Shule ya Sekondari Kiwanja, hadi tarehe 18 Oktoba 2019. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Pia, Chalamila ameagiza kila mwanafunzi katika shule hiyo kulipa Sh. 200,000, huku wengine wanaodaiwa kuchoma moto mabweni ya shule hiyo, kulipa Sh. 500,000 kila mmoja.

Chalamila ametoa adhabu hiyo ili kufidia gharama za ujenzi wa mabweni ya shule, yanayodaiwa kuchomwa moto na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.

Mkuu huyo wa mkoa ametoa adhabu hiyo leo tarehe 4 Oktoba 2019, alipotembelea shule hiyo kwa mara ya pili, baada ya jana kuwatandika viboko wanafunzi 14, wanaodaiwa kuhusika katika tukio la kuchoma moto mabweni.

“Nilipanga niwatandike kweli kweli ,mlambe mchanga na kokoto mmeze. Ili mtaje vizuri waliofanya hivyo, lakini itoshe kusema leo mtaondoka kurudi kwa baba zenu na mama zenu, na mikono ikiwawasha ili mkachome nyumba za baba na mama zenu,” amesema Chalamila na kuongeza;

“Mliochoma mabweni, nawaambia kama mna hamu na mnawashwa kuchoma vitu, mkachome nyumba za baba zenu. Kuanzia sasa nafunga form 5 na 6, mnaondoka kwenda kwenu, na ikifika saa 4 bado mnang’ang’a hapa, mtakung’utwa kichapo cha kufa mtu.”

Chalamila ameeleza kuwa, mwanafunzi atakayeshindwa kulipa fedha hizo kabla ya muda husika, atachukuliwa hatua ikiwemo kuzuiwa kufanya mtihani wa kumalizia kidato cha sita.

“Mtu yeyote ambaye hataingiza pesa kabla ya tarehe 18 na kuja kuripoti shule, utafuatwa na pingu huko huko uliko. Na jambo la pili, tutakukuzuia hautafanya mitihani tena ya kidato cha 6 katika maisha yako mpaka unaingia kaburini,” amesema Chalamila.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

error: Content is protected !!