KLABU ya Azam FC imethibitisha kuwa mpaka sasa hawajafanya mazungumzo yoyote na Haruna Niyonzima ambaye ni mchezaji wa timu ya Simba baada ya kuwapo kwa tetesi kuwa huwenda akatimka ndani kikosi hicho. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).
Niyonzima ambaye amekuwa katika wakati mgumu tangu alipojiunga na Simba katika msimu uliopita, hajaonekana mara nyingi uwanjani katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuwa katika majeruhi yaliyomuweka nje kwa muda mrefu na kuingia katika mgogoro na uongozi wa klabu hiyo.
Msemaji wa Azam FC, Jafari Idd amesema kuwa mpaka sasa hawajafanya mazungumzo na mchezaji huyo, lakini bado kwao dirisha lipo wazi na kama mwalimu atamuhitaji mchezaji wowote basi hawatosita kumchukua.
“Hao wachezaji bado hatujazungumza nao lakini huu ni mchezo wa mpira na lolote linaweza kutokea, sisi dirisha lipo wazi tuna msikiliza mwalimu anamuhitaji nani kama ni ndani ya nchi au nje ya nchi sisi tunamchukua tunampa mkataba.
“Naomba tuwaondoe presha wenye timu zao mwalimu akisema anamtaka yoyote kwenye klabu yoyote tutafanya naye mazungumzo na tutamchukua ili tupate huduma yake, lakini tunaomba hawa wachezaji wawe huru maisha yaona klabu zao ziondoe fikra hizo kwa sasa,” alisema Jafari Idd.
Azam FC ambao baada ya kufungiliwa kwa dirisha dogo la usajiri hapo jana, tayari walisha ingia kandarasi ya mwaka mmoja na mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Obrey Chirwa na huwenda wakafanya usajiri wa wachezaji wengi zaidi katika dirisha ili la usajili.
Leave a comment