Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa AZAKI zapeleka fikra mpya Ofisi ya Msajili
Habari za Siasa

AZAKI zapeleka fikra mpya Ofisi ya Msajili

Spread the love

ASASI za Kiraia (AZAKI) nchini zimemshauri Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kuunda Kamati Huru itakayoshughulikia tuhuma zinazokikabili Chama cha ACT-Wazalendo, badala ya kutishia kukifuta. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 1 Aprili 2019 jijini Dar es Salaam, na Mwanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Said Suleiman wakati akisoma tamko la AZAKI  hizo zipatazo 65.

Suleiman amesema, AZAKI hizo zimemshauri Jaji Mutungi kuanzisha tume hiyo itakayohusisha makundi huru, ikiwemo AZAKI ili kuchambua tuhuma zinazokabili ACT-Wazalendo kwa minajili ya kutenda haki kwa pande zote.

“Barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa yenye kumbukumbu HA.322/362/2D/98 ya nia ya Msajili wa Vyama vya Siasa kufuta usajili wa kudumu wa chama cha ACT Wazalendo imeleta mkanganyiko miongoni mwa Tanzania.

 Kwa nchi yetu ambayo ni ya Kidemokrasia inayofuata misingi ya haki na uwazi tusingetegemea Msajili wa Vyama vya Siasa akitoa onyo kali la namna ile kwa tuhuma ambazo hazijathibitika badala yake angetafuta namna nzuri ya kuwaita na kusuluhisha kabla ya kufikiria kuchukua hatua za awali kama mlezi wa vyama vya saisa.  Barua hii ilitolewaa mapema na kubeba shutuma nyingi ambazo zingeweza kujadiliwa kati ya chama husika na ofisi ya msajili.”

“Msajili wa vyama vya siasa tunamshauri badala ya kufikiria kuifuta ACT  Wazalendo baada ya siku 14, aunde Kamati Huru itakayojumuisha makundi mengine huru, wakiwemo wana AZAKI kuchambua ukweli wa tuhuma zilizokwenda kwa ACT-Wazalendo ili kutenda haki kwa pande zote. Lengo iwe ni kujenga na si kujenga chuki na uhasama zaidi,” amesema Suleiman.

Suleiman amemshauri Jaji Mutungi kutumia vyombo mbalimbali ikiwemo Baraza la Vyama vya Siasa, Kituo cha Demokrasia na viongozi wa dini katika kutatua changamoto anazokabiliana nazo kwenye uendeshaji wa vyama vya siasa nchini badala ya kuamua kila jambo pasina kushirikisha wadau hao.

 “Msajili wa Vyama vya Siasa aache kuvitisha na kuingilia migogoro ya ndani ya vyama vya siasa na badala yake aongozwe zaidi na hekima katika kusimamia misingi ya demokrasia na haki za wananchi wote kujiunga katika vyama wanavyovitaka bila kuwekewa vikwazo visivyotambulika na sheria za nchi yetu,” ianeleza sehemu ya tamko hilo.

 Aidha, AZAKI hizo zimemuomba Rais John Magufuli kukutana na vyama vya siasa vya upinzani ili kukaa katika meza ya mazungumzo kuhusu malalamiko yao mbalimbali.                   

 “Kwa kuwa lengo letu ni kujenga na si kubomoa, na pia kwakuwa AZAKI ni wadau wakubwa wa maendeleo,  kama itampendeza Mhe Rais tunaomba kuwa na mkutano wa pamoja na yeye ili tuweze kushauriana naye mambo mengi ya kitaifa ikiwemo hili la demokrasia na uhuru wa raia na vyama vyao.

“Tunaamini demokrasia na siasa ndio msingi na ustawi wa taifa lolote nchini hivyo hatuna njia ya kukwepa kuzungumzia,” imeleza sehemu ya tamko la AZAZKI hizo.

Katika hatua nyingine, AZAKI hizo zimetoa wito kwa serikali kurekebisha baadhi ya vifungu vya sheria mpya ya vyama vya siasa vyenye mapungufu ili kutoa uwanja sawa na huru wa kufanya siasa nchini.

 “Endapo itashindikana hivyo tunashauri AZAKI, Watetezi wa haki za binadamu  au vyama vya siasa viende mahakamani kuiomba mahakama itengue vipengele vyote kandamizi.

“Wakati huo huo tunashauri mifumo yetu ya haki hapa nchini kuzingatia sana haki za binadamu wanapokuwa wanatoa maamuzi yao katika mambo mbali yenye maslahi kwa Taifa,” limeeleza tamko hilo.

AZAKI hizo zimefikia hatua ya kutoa wito huo kwa serikali kwa kile ilichoeleza kuwa, haki za demokrasia na uhuru wa kujumuika na kujiunga na vyama vya siasa nchini inazidi kuzorota kila kukicha.

 “Kwetu sisi hali hii tunaitafsiri kama ni mwazo wa kubomoa umoja wa kitaifa na kupoteza amani ya nchi. Ipo mifano kadhaa inayo akisi hali duni ya sasa ya demokrasia nchini,” limeeleza tamko hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

error: Content is protected !!