Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Askofu: Mivutano ya dini na serikali iangaliwe
Habari za Siasa

Askofu: Mivutano ya dini na serikali iangaliwe

Askofu wa Anglikana Dayosisi ya Tanga, Maimbo Ndolwa
Spread the love

KUMEKUWEPO na mifutano baridi kati ya taasisi za dini na serikali hasa katika utoaji wa huduma za kijamii jambo ambalo linasababisha kuwepo kwa taswira hasi. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza kwenye Kikao cha Rais John Magufuli na viongozi wa dini Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 23 Januari 2019, Askofu wa Anglikana Dayosisi ya Tanga, Maimbo Ndolwa amesema serikali inapaswa kuangalia namna ya kuondoa mkanganyiko huo.

“Kuna mambo mawili nayaona kama changamoto na yakifanyiwa kazi, tutaendelea kwenda pamoja. Mashirika ya dini yanawajibika kwa raia kama ambavyo serikali inawajibika kwa raia wake, kwa namna hiyo ya kuwajibika kwa pamoja, tulikubaliana kufanya kazi kwa pamoja katika sekta mbalimbali.

Ametoa mfano kwamba, serikali imekuwa ikijenga hospitali ama vituo vya afya karibu na vile vilivyojengwa na taasisi za dini mwendo mchache kutoka hospitali ya kituo cha dini na kusababisha mkanganyiko.

Askofu Ndolwa ameiomba serikali kuelekeza huduma hizo maeneo ya mbali ambayo yanahitaji huduma hizo badala ya kuziweka pamoja na kusababisha walio kwenye maeneo ya mbali kukosa huduma hizo.

“Siku za karibuni kumetokea kuvutana hasa kwenye ngazi ya wilaya, utakuta mahali shirika la dini limekubaliana na serikali kujenga hospitali lakini serikali imejenga hapo hapo.

“Ushauri wangu, kungekuwa na forum (jukwaa) mara kwa mara ya mambo haya kwa sababu serikali inawajibika na mashirika ya dini yanawajibika, sisi kutoa huduma ya afya ya elimu ni wajibu wetu kwa kuwa ni ibada,” anasema.

Akizungmzia kwenye elimu Askofu Ndolwa amesema, kumekuwa na mivutano katika eneo hilo kati ya mashirika ya dini na serikali hivyo safari ya utoaji elimu kuwa ngumu.

Alinikisa Cheyo, Askofu wa Kanisa la Monrovian, yapo matatizo makubwa kwenye suala la usambazaji maji na kwamba, serikali inapaswa kuliangalia hilo kutokana na umuhimu wake.

“Tatizo la maji katika nchi yetu ni kuwa sana, umeme kwa asilimia kubwa umeenea lakini kwa upande wa maji kuna tatizo kubwa. Kwa kuwa maji ni uhai, kungetumika namna fulani angalau kijiji kingekuwa hata na bomba moja,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!