Thursday , 18 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Askofu Kakobe: Wanataka tumtenge Askofu Gwajima
Habari Mchanganyiko

Askofu Kakobe: Wanataka tumtenge Askofu Gwajima

Spread the love
  1. ZACHARY Kakobe, Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Felloship (FGBF) amedai, upo mpango wa kumtenganisha Josephat Gwajima, Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima na viongozi wengine wa dini. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Amedai kuwa, video ya ngono inayodaiwa kuwa ni ya Askofu Gwajima, imetengenezwa ili aonekane kuwa mzinzi hivyo viongozi wenzake wamtenge.

Akizungumza katika ibada iliyofanyika katika Kanisa la Ufufuo na Uzima, Ubungo jijini Dar es Salaam leo tarehe 12 Mei 2019, Askofu Kakobe amemtetea Gwajima kwamba, anachafuliwa kwa makusudi.

Amedai kuvuja kwa video hiyo, kumetokana na hatua ya Askofu Gwajima kurudisha uhusiano wake na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Na kwamba, hatua hiyo imesababisha baadhi ya watu, hasa wanaochukizwa na kurejea kwa uhusiano huo wa Makonda na Gwajima, kuvujisha video ya ngono kwa ajili ya kumkomoa.

“Aliyeanzisha hili suala, aliwaza katika umoja wetu tutamuangalia Gwajima kama mzinzi, halafu tumtenge. Kwa taarifa yenu, nimempenda huyu sasa kuliko wakati wowote, waswahili wanasemaje, mwenye wivu ajinyonge,” amesema Askofu Kakobe na kuongeza;

“Wakajaribu kupeleka hizo fitina mpaka kwa Makonda, naye kwa sehemu akataka kukubaliana nao lakini naye ameshtuka, anaona kumbe wapo watu wana biashara ya mfarakano wao, naye alishtuka ndugu zangu.”

Askofu Kakobea amesema, hawawezi kuwatenga wale wanaofikiriwa kuwa na dhambi na kuwa, wakitengwa watu hao wanakuwa hawajasaidiwa.

“Hatuwezi kuwatenga wale mnaofikiri wana dhambi, na sisi kama wazee, kama Makonda ana upungufu, sisi si wanasiasa ni watumishi wa Mungu, tukimtenga tutamsaidiaje?” amehoji.

Aidha, Askofu Kakobe amewataka watu wenye ushahidi wa moja kwa moja ya kwamba, Askofu Gwajima alihusika katika video hiyo ajitokeze hadharani, na kama hayupo basi watu waache kumtuhumu kiongozi huyo wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.

Askofu Kakobe amewataka waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kupuuza tuhuma hizo “wakati wa kila kiuongo kufanya kazi peke ake umepita, wakati huu ukimgusa mmoja umegusa wote uksishambulia mmoja umegusa wote.

“Kwa hiyo wamegusa moto. Waumini msitange tange, usitafute kuja kwangu wala kwa yeyote hapa uko mahala salama,” amesema Askofu Kakobe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!