Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Askofu Bagonza awataka waumini kuwa makini
Habari Mchanganyiko

Askofu Bagonza awataka waumini kuwa makini

Spread the love

DK. Benson Bagonza, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe, mkoani Kagera, amewataka waumini na wananchi kuwa makini na wanaojinadi kuwatetea. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Amesema, katika kipindi hiki ambacho kuna ubadhirifu mkubwa wa mali ya umma, lazima wapatikane watu ambao wanaweza kutetea hata kama watatukanwa na kubezwa.

Dk. Bagonza ametoa kauli hiyo leo tarehe 20 Aprili 2019 19, 2019 katika Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika kitaifa kwenye Kanisa la KKKT, Dayosisi ya Karagwe.

Mbele ya waumini wa kanisa hilo Dk. Bagonza amesema, wapo wanaojifanya wanatetea wanyonge, kumbe wanajineemesha.

Kiongozi huyo amesema, unyonge, maradhi na umasikini wa Watanzania umegeuzwa mtaji wa wasaka tonge.

Na kwamba, kwa sasa jamii ina kilio kikubwa cha rushwa, rushwa, ujinga na ubadhirifu wa mali ya umma kila kukicha.

“Kuna kilio kikubwa cha umasikini, maradhi na ubadhirifu wa mali za umma. Lazima wapatikane watu walio tayari kuteseka kwa ajili ya kukomesha madhambi hayo,” amesema Dk. Bagonza.

Amewaambia waumini wa kaniza hilo na wananchi kwa ujumla kwamba, umasikini wa Watanzania haupaswi kuwa mtaji wa wasaka tonge.

“Wala wanaojitokeza kutetea wanyonge lazima wawe makini kutotumia unyonge wetu kujinufaisha kiuchumi, kisiasa na hata kiimani,” amesema.

Dk. Bagonza amesema, katika mazingira haya lazima watokee watu watakaotukanwa, kuitwa majina mabaya, waandikwe vibaya magazetini na mitandaoni, lakini naamini Mungu hawezi kuwaacha,” amesema.

Ameeleza kushangazwa na wanasiasa wanaohama kwa madai ya kuunga mkono maendeleo, wakati maendeleo hayana chama.

Amesema, kuna maneno matatu yanasisitiza upendo wa Mungu kwa wanadamu.

Amesema kwamba, and Mungu aliwapenda wanadamu kuliko mwanaye, upendo wa ajabu wa kutoa na siyo kupokea.

Na kwamba, kwa misumari tu Yesu Kristo angedondoka kwa maumivu pale msalabani, lakini upendo ndiyo ulimuweka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!