Tuesday , 19 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Ashitakiwa kwa uhujumu uchumi, kisa kudhamini kesi ya vipodozi
Habari Mchanganyiko

Ashitakiwa kwa uhujumu uchumi, kisa kudhamini kesi ya vipodozi

Spread the love

MKAZI wa mtaa wa Uzunguni wilaya ya Muleba, Kagera, Alex Chacha anasota katika gereza la Butimba Mwanza kwa tuhuma za uhujumu uchumi baada ya kumdhamini mmoja wa watuhumiwa wa kesi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Watuhumiwa wanne waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uingizaji na uuzaji wa vipodozi vilivyopigwa marufuku ni Sendi Wambura, Kasongo Otiang`a, Elisha Albetus na Charles Marwa.

Watuhumiwa hao kwa sasa wamefunguliwa kesi ya uhujumu uchumi baada ya kuwepo tuhuma za kusafirisha madini kupitia uwanja wa ndege wa Mwanza kwenda nchini Kenya bila kuwa na vibali.

Inaelezwa  Alex Chacha mwaka 2015 alimdhamini Kasongo Otiang`a aliyekuwa akishtakiwa yeye na wenzake watatu ambao wametajwa hapo juu kwa makosa mbalimbali ya kukutwa na vipodozi kupitia kesi namba 97 ya 2015,

Inaelezwa watuhumiwa hao wa kesi namba 97 walipata dhamana baada ya kukidhi masharti ya dhamana yaliokuwa yamewekwa na mahakama ya wilaya ya Bukoba licha ya wakili wa serikali Athman Matuma kupinga dhamana hiyo.

Hata hivyo kufuatia wakili wa serikali kutoridhika na dhamana hiyo, alikata rufaa Mahakama Kuu kanda ya Bukoba kupitia rufaa namba 13 ya 2016 ambako rufaa hiyo Novemba 4 mwaka 2016 ilitupiliwa mbali na watuhumiwa kuruhusiwa kuendelea na dhamana yao.

Pia wakili huyo wa serikali hakuridhika na uamzi huo na kuamua kwenda kukata rufaa mahakama ya rufani Tanzania kupinga uamzi wa Mahakama Kuu kanda ya Bukoba kupitia rufaa namba 480 ya 2016.

Agosti 24 mwaka huu Mahakama ya Rufaa ilitupilia mbali tena rufaa hiyo na kuamuru watuhumiwa wote kuendelea na dhamana kama ilivyotolewa na Mahakama ya wilaya ya Bukoba.

Inadaiwa kuwa  baada ya wakili wa serikali kuona imeshindikana aliamuru watuhumiwa wote wakamatwe akiwemo na mdhamni wa Kasongo Otiang`a aliyekuwa amefika mahakamani hapo kusikiliza kesi hiyo ambaye ni Alex Chacha.

Inaelezwa kuwa Wakili Matuma baada ya kuagiza watuhumiwa hao wakamatwe aliwafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi namba 5 ya 2018 kwenye mahakama ya hakimu mkazi Bukoba kwa madai ni maelekezo kutoka jeshi la polisi mkoa wa Mwanza.

Taarifa zinaonyesha kuwa jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza liliwafunguliwa watuhumiwa hao jalada lenye kumbukumbu namba MW/ IR/ 256 ya 2018.

Ndugu wa Alex Chacha wafunguka

Mmoja wa ndugu wa Alex Chacha, anayefahamika kwa jina la Paul Matiku ameueleza mtandao huu kuwa Agousti 26 mwaka huu watuhumiwa wote walifuatwa na askari Polisi kutoka Mwanza na Agousti 27 mwaka huu walifikishwa mwanza.

Matiku alisema, baada ya watuhumiwa hao kufikishwa Mwanza, moja kwa moja walipandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mwanza na kusomewa mashtaka kupitia Economic case No. 8 ya 2018.

“Sisi kama ndugu wa Alex Chacha tunaamini kabisa kwamba ndugu yetu anajishughulisha na uvuvi wa samaki katika kisiwa cha Kerebe kilichopo wilaya ya Muleba.

“Ndugu yetu tunafahamu alikuwa hatafutwi  jeshi la Polisi kupitia kesi yenye kumb. Namba MW/ IR/ 2561/ 2018 na kabisa kinachoonekana ni mambo binafsi baina yake na wakili wa serikali,” alisema Matiku.

Alisema wakili wa serikali aliamua kutumia mamlaka yake vibaya kumbambikizia kesi hiyo ili kumkoamoa na wala sio kwa maslahi ya haki nay a Taifa.

Matiku aliiomba serikali kupitia kwa waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Kangi Lugola kuingilia suala hilo kwani ni wazi kwamba ndugu yake kaonewa, hatua ambayo alidai itasaidia kutenda haki.

Matiku alisema wao kama ndugu tayari wamemuandikia barua kamanda wa Polisi mkoa (Jonathan Shanna) kuomba kuchunguza upya jarada hilo, pia wameandika barua kwenda kwa mkuu wa usalama wa Taifa mkoa pamoja na kwa mkuu wa mkoa huo

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna alipotafutwa na mtandao huu kuhusu kuwepo kwa taarifa za kukamatwa kwa Alex Chacha na wenzake alikiri watuhumiwa hao kukamatwa.

“Nikweli walikamatwa na walifunguliwa kesi na huyo ambaye unasema amebambikiziwa kesi, ni miongoni mwa watu ambao tulikuwa  wanatafutwa na jeshi la Polisi na kama unaona kaonewa mtafute wakili (Athmana Matuma),” alisema Shanna.

Wakili wa serikali Athman Matuma ambaye aliagiza Alex Chacha akamatwe, alipotafutwa na mwandishi wagazeti hili, kwa siku nne kwa nyakati tofauti kupitia simu yake ya mkononi namba (zinahifadhiwa) simu yake iliita bila majibu.

Pia wakili huyo hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno ulioelezea madai hayo, kwenye simu yake ya mkononi, haukujibiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Diwani, wananchi wengine 463 wahama Ngorongoro

Spread the loveMakamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ambaye pia...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Shule zafungwa kutokana na ongezeko la joto

Spread the loveSUDAN Kusini imeamuru kufungwa kwa shule zote kuanzia leo Jumatatu,...

Habari Mchanganyiko

Bunge laja na Marathon kuchangia ujenzi wa sekondari

Spread the loveBUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia kukusanya fedha...

error: Content is protected !!