Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (kulia) akipokea maziwa aina ya Asas Dairies Milk kutoka kwa Mshauri wa Kampuni hiyo, Abdul Ally

ASAS wagawa maziwa kwa Wabunge kuhamasisha unywaji

WATANZANIA wamehamasishwa kutumia maziwa kwa wingi ili kuweza kutunza afya zao kutokana na kuwa maziwa hayo yanapaikana. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Wito huo umetolewa na Mshauri wa Kampuni ya Asas Dairies Milk, Abdul Ally wakati akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega pamoja na baadhi ya wabunge akiwemo mbunge wa Viti Maalum, Mariam Ditopile (CCM). 

Akizungumza kuhusu matumizi ya maziwa alisema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikizalisha maziwa ambayo kimsingi yameboreshwa sambamba na kusambaa katika nchi nzima.

Amesema kuwa kwa sasa kampuni hiyo imekuwa ikifanya kampeni ya kusambaza maziwa hayo katika taasisi mbalimbali ikiwa pamoja na kusambaza katika shule za msingi na sekondari.

Naye mwakilishi wa Kampuni hiyo mkoa wa Dodoma, Lupyana Chagula, alisema kampuni hiyo imeona ni vema kupeleka maziwa bungeni ili kuhamasisha unywaji wa maziwa sambamba na kuchochea matumizi ya mazao ya maziwa ambayo ni bidhaa za ndani badala ya kusubiri bidhaa hiyo kutoka nje.

Kwa upande wake, Waziri Ulega alisema kampuni hiyo imekuwa ikijitahidi kuhamasisha unywaji wa maziwa na yamekuwa yakipendwa na wanywaji na kusababisha kuongeza hamasa ya unywaji wa maziwa kwa jamii.

WATANZANIA wamehamasishwa kutumia maziwa kwa wingi ili kuweza kutunza afya zao kutokana na kuwa maziwa hayo yanapaikana. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea). Wito huo umetolewa na Mshauri wa Kampuni ya Asas Dairies Milk, Abdul Ally wakati akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega pamoja na baadhi ya wabunge akiwemo mbunge wa Viti Maalum, Mariam Ditopile (CCM).  Akizungumza kuhusu matumizi ya maziwa alisema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikizalisha maziwa ambayo kimsingi yameboreshwa sambamba na kusambaa katika nchi nzima. Amesema kuwa kwa sasa kampuni hiyo imekuwa ikifanya kampeni ya kusambaza maziwa hayo katika taasisi mbalimbali ikiwa pamoja na…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Danson Kaijage

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram