Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Tangulizi Arusha, Tanzania yazizima, kuaga miili 36
Tangulizi

Arusha, Tanzania yazizima, kuaga miili 36

Baadhi ya miili ya marehemu 36 yakiwa kwenye majeneza tayari kwa kupewa heshima ya mwisho
Spread the love

TAYARI zoezi la kuaga miili 36 ambayo ni ya wanafunzi 33, walimu 2 na dereva wao waliofariki katika ajali ya gari Karatu mkoani Arusha limekamilika likiongozwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini humo, anaandika Hamisi Mguta.

Wanafunzi hao ambao ni wa shule ya msingi Lucky Vicent waliokuwa wakisafiri kuelekea katika mitihani ya ujirani mwema katika shule ya Tumaini walipata ajali katika eneo la Rhotia Marera wakiwa njiani.

Tukio hilo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Elimu nchini Kenya, Fred Matiang’i, Katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa na mwenyeji wao Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo.

Kauri za viongozi mbalimbali katika kuaga miili hiyo

Samia Suluhu

“Nimesimama hapa kwa niaba ya Rais John Magufuli amenituma nije kutoa pole kwa familia za wanafunzi, walimu na dereva. Sisi wazazi na taifa kwa ujumla tulikuwa na mipango mikubwa kwa watoto hawa, lakini tukumbuke kazi ya Mungu haina makosa, tumuombe mwenyezi Mungu azilaze mahali pema peponi roho za Malaika hawa, walimu na dereva.”

Samia Suluhu akitoa salamu zake za mwisho kabla ya kuaga miili hiyo

Fred Matiang’i

“Nimekuja hapa siku ya leo, nimetumwa na Rais wetu Uhuru Kenyata nilete salamu za rambirambi zake binafsi na mkewe pamoja na kutoka serikali ya Kenya na wananchi wa nchi jirani yenu.

“Tulihuzunika sana tulipopata habari ya ajali hii na tumekuja kuomboleza na kushirikiana kwa maombi na kusema pole kwa kilichotokea.”

Joyce Ndalichako

“Nasikitika sana kama Waziri wa Elimu kwa sababu vijana hawa wamefariki wakiwa katika harakati za kujiandaa na mtihani wa Taifa.”

Freeman Mbowe

“Tutafakari amani yetu, tutafakari ushirikiano wetu kupitia maamuzi ya mwenyezi mungu kuzitoa roho za wapendwa wetu watoto, wapendwa wetu walimu katika ajali iliyotokea kule Karatu.

“Ningependa kutoa pole kwa niaba ya Chadema na vyama vyote vya upinzani na kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kuwapa pole sana kwa familia za marehemu wote, serikali, wananchi wa Arusha na Watanzania wote ambao msiba huu umekuwa na mshituko mkubwa sana kwa taifa kiujumla, Bwana ametoa na Baba ametwaa jina lake lihimidiwe.”

Mmoja wa wazazi wa marehemu akitoa heshima ya mwisho

Abdulrahman Kinana

“Natoa salamu za rambirambi kwa niaba ya wana CCM na viongozi na wabunge, sisi sote ni waumini wa dini kama kuna kitu kinatuunganisha kwa pamoja dini zote na madhehebu yote ni pamoja na kifo, sote tunaamini kwamba kila binadamu atakuwa na mwisho.

“Nichukue nafasi hii kuwapa pole wazazi, viongozi wa mkoa wa Arusha. Asanteni sana.”

Wanafunzi wa shule ya Lucky Vicenty wakiingia uwanjani kutoa heshima ya mwisho kwa wenzao

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CDF Mabeyo: Magufuli alijua anakufa

Spread the love  ALIYEKUWA Mkuu wa Majeshi nchini (CDF), Jenerali Venance Mabeyo,...

AfyaTangulizi

Serikali yafafanua kuondolewa dawa 178 kitita cha NHIF

Spread the loveSERIKALI imesema imeondoa dawa 178 katika kitita cha Mfuko wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ateua, amtumbua Kamishna Ngorongoro

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na utenguzi wa...

Tangulizi

5 mbaroni madai ya Makamba kumng’oa Samia 2025

Spread the loveWATU watano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya...

error: Content is protected !!