January 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Arsenal waipiga Chelsea, watwaa ubingwa FA CUP

Spread the love

PIERRE- Emerick Aubameyang, kiungo mshambuliaji wa Arsenal ameiwezesha timu yake kutwaa ubingwa wa Kombe la FA CUP nchini Uingereza kwa kuofungia magoli 2-1 dhidi ya Chelsea. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea)

Aubameyang amefunga magoli hayo moja kwa penati dakali ya 28 baada ya kuchezewa rafu ndani ya 18 na beki wa Chelsea Cesar Azpilicueta na kuzawadiwa kadi ya njano.

Goli hilo lilikuwa la kusawazisha baada ya Chelsea kuongoza Christian Pulisic kufunga dakika ya 5 ya mchezo huo uliopigwa dimba la Wembley.

Dakika ya 68, Aubameyang raia wa Gabon aliifungia Arsenal goli la pili akipokea pasi safi kutoka kwa Nicholas Pepe.

Chelsea iliwalazimu kucheza wakiwa pungufu kuanzia dakika ya 72 baada ya kiungo wake, Mateo Kovacic kuzawadia kadi ya pili ya njano kwa kumchezea rafu kiungo wa Arsenal, Granint Xhaka.

Arsenal wametwaa taji hilo kwa mara ya 14 ambapo mara ya mwisho ililitwaa taji hilo mwaka 2017.

error: Content is protected !!