Emmanuel Amunike, Kocha wa Taifa Stars

Amunike bado awapa nafasi wachezaji wa Simba

KATIKA keulekea mchezo dhidi ya Uganda unaotarajia kuchezwa Septemba 8, 2018 Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars,’ Emannuel Amunike amesema wachezaji aliowatimua kwenye kikosi hicho bado ni sehemu ya timu hiyo licha ya kusisitiza swala la nidhamu katika timu hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Amunike ambaye ataiongoza kwa mara ya kwanza Stars kwenye mchezo huo dhidi ya Uganda amesema kuwa kuna wachezaji walioitwa timu ya taifa lakini kuna maamuzi yaliyofanyika hivyo haimaniishi kuwa siyo sehemu ya timu.

“Sote tunafahamu kwenye kila taasisi tunasisitiza nidhamu pamoja na uwajibikaji, jopo la makocha tumeshawaeleza timu ya taifa ni kwa ajili ya kila mtanzania na ni fahari ya watanzania,” amesema Amunike.

Amunike aliongezea ya kuwa kila mchezaji aliyeitwa timu ya taifa ni muhimu na anakitu cha kuchangia kwenye timu kwa hiyo kama kuna mchezaji haumuoni siyo kama amekataa au hana uwezo.

Kwa upande wa Nahodha wa kikosi hicho, Mbwana Samatta amesema kuwa mwisho wa siku lazima tukubaliane na hali halisi, tunakwenda kwenye mchezo hakuna muda wa kuyazungumzia mambo ambayo hayawezi kutusaidia kwenye Mechi hiyo.

KATIKA keulekea mchezo dhidi ya Uganda unaotarajia kuchezwa Septemba 8, 2018 Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars,' Emannuel Amunike amesema wachezaji aliowatimua kwenye kikosi hicho bado ni sehemu ya timu hiyo licha ya kusisitiza swala la nidhamu katika timu hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea). Amunike ambaye ataiongoza kwa mara ya kwanza Stars kwenye mchezo huo dhidi ya Uganda amesema kuwa kuna wachezaji walioitwa timu ya taifa lakini kuna maamuzi yaliyofanyika hivyo haimaniishi kuwa siyo sehemu ya timu. “Sote tunafahamu kwenye kila taasisi tunasisitiza nidhamu pamoja na uwajibikaji, jopo la makocha tumeshawaeleza timu ya taifa ni…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Kelvin Mwaipungu

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube