Tuesday , 16 April 2024
Home Kitengo Michezo Amunike awajia juu wanaobeza mfumo wake
Michezo

Amunike awajia juu wanaobeza mfumo wake

Emmanuel Amunike, Kocha wa Taifa Stars
Spread the love

KUELEKEA kwenye mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu kwa kombe la mataifa Afrika dhidi ya Uganda, kocha mjuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Emanuel Amunike amewajia juu wale wote wanaobeza aina ya mfumo wa uchezaji anao utumia ndani ya kikosi hicho bila kuangalia sifa za wachezaji. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea)

Kocha huyo amezungumza hayo mbele ya waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kesho na kusema kuwa muda mwengine mfumo sio shida, bali sifa za wachezaji watakaoweza kuendana na mfumo huo ndio muhimu.

“Watu wengi wanaongelea kuhusu mifumo kwa Mfano (3-5-2) (4-1-4-1) muda mwingine kuwa na wachezaji wenye sifa inayoendana na mifumo hiyo ndio muhimu zaidi” alisema Emmanuel Amunike

Hali hiyo ilitokea baada ya Tanzania kufungwa katika mchezo wa kundi L dhidi ya Lesotho kwa bao 2-0 na lawama zote kumuangukia yeye ambaye ndio mkuu wa benchi la ufundi kwa kushindwa kuipanga timu yake vizuri.

Katika kuelekea mchezo dhidi ya Uganda Amunike alisema kuwa kuwa katika mchezo wa kesho hautakuwa mwepesi kwa kuwa Uganda hawajaja hapa kulala ingawa wameshakata tiketi ya kushiriki michuano hiyo June, 2019 nchini Misri.

Tanzania inahitaji ushindi wa hali na mali katika mchezo huo ili iwese kufanikiwa kufuzu kwa michuano hiyo baada ya kupita miaka 39 toka mara ya mwisho ilipo shiriki michuano hiyo 1980 nchini Nigeria.

 

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

Michezo

TFF, Amrouche ngoma nzito

Spread the loveVIPENGELE vya mkataba wa kazi aliotia saini Kocha Mkuu wa...

error: Content is protected !!