Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Aliyeshinda ubunge Chadema asema…
Habari za Siasa

Aliyeshinda ubunge Chadema asema…

Spread the love

AIDA Joseph Khenani, mbunge mteule wa Nkasi Kaskazini kupitia Chadema amesema, ushindi wake umejaa majonzi kutokana na kile kilichotokea kwa wagombea wenzake wa upinzani. Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Aida ametoa kauli hiyo leo Ijumaa tarehe 30 Oktoba 2020 wakati akizungumza na MwanaHALISI Online kwa simu kupata mtazamo wake kutokana na kuwa mgombea pekee mpaka sasa wa Chadema aliyeibuka mshindi.

Matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatano ya tarehe 28 Oktoba 2020 yanaonyesha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimejikusanyia majimbo zaidi ya 233 kati ya 264.

Hadi kufikia saa 2 usiku usiku, upinzani ulikuwa umeshinda majimbo mawili hilo la Aida aliyemshinda Ally Kessy wa CCM.

Aida amemshinda Kessy aliyekuwa akiongoza jimbo hilo kwa miaka kumi mfululizo kwa kura 21,226 huku Kessy akipata kura 19,972.

Jimbo jingine ni la Mtwara Vijijini ambapo, Shamsia Mtamba wa CUF amemshinda Hawa Ghasia wa CCM aliyekuwa akitetea nafasi hiyo.

Vyama vya Chadema na CUF vimeshuhudia wabunge wake wakianguka kwenye uchaguzi huo akiwemo aliyekuwa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, Freeman Mbowe katika Jimbo la Hai.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Aida amesema “namshukuru Mungu kwa kuibuka mshindi, lakini ushindi wangu umekuwa si wa furaha sana kwa yale yaliyotokea kwa wagombea wenzangu.”

“Wameondoa wapinzania bungeni, hii ni hatari sana na hiki kilichofanyika Watanzania wana akili timamu ya kujua nini kimetokea na ni wakati wa Watanzania tufanye tafakari kubwa,” amesema Aida anayerejea bungeni akiwa mbunge wa jimbo kutoka wa viti maalum katika bunge lililopita.

Akijibu swali la ugumu anaouna kwenda katika Bunge lijalo, Aida amesema “mimi sioni shida sana kama wote tukijua tumekwenda bungeni kufanya nini ingawa upekee wangu utakuwa ni changamoto kubwa na kila nitakachokuwa nafanya nitafuata maelekezo ya chama change.”

Amesema, “CCM wanaweza kubadilika chochote wanachokitaka, lakini kunapokuwa na utofauti kama bunge lililopita, walikuwa wanashindwa.”

Mbunge huyo mteule aliyezaliwa Januari 20 mwaka 1990 amesema “Aida huyu anayekwenda bungeni, haangalii amekwenda na nani. Lakini Watanzania tufanye tafakuri ya kutosha, waangalie hivi wabunge wa CCM ndiyo bora zaidi?”

Akizungumzia wabunge wenzake walioshindwa amesema “nilitamani sana kuendelea kujifunza kutoka kwao, uwepo wao bungeni, nitakavyowamisi sana, Watanzania watamisi michango yao iliyokuwa bora kwa manufaa ya Taifa.”

“Mimi Aida napenda kujifunza kwa kila mtu, mtoto, mkubwa na yoyote, nitawamisi sana viongozi wangu wa kambi. Nilikuwa najifunza kwa dada zangu waliotoka viti maalum na kuwa wabunge wa jimbo, lakini sasa hilo nitalikosa,” amesema

MwanaHALISI Online lilipotaka kujua iwapo chama chake kikiamua kutokushiriki kwenye Bunge hilo na kumtaka yeye mwenyewe kujitoa, Aida amesema;

“Siwezi kuwa na jibu la haraka, lakini mimi ni mwanachama wa Chadema, kilichotokea kimekikumba chama, kwa uamuzi wowote utakuwa shirikishi, kamati kuu naiheshimu na pamoja na uamuzi, mimi nimechaguliwa na watu.”

“Pia nina viongozi ngazi ya chini, hivyo kabla ya kufanya uamuzi, wataangalia athari zake na mwisho nafikiri uamuzi utakuwa sahihi,” amesema Aida.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!