Alichokisema Kikwete baada ya Mwana FA kuzindua pafyumu

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amempongeza mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ kwa kuanzisha bidhaa yake ya mafuta ya kunyunyuzia mwilini ‘Body Spray’. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Dk. Kikwete amempongeza kwa kuandika kuwa, amefarijika kutokana na mwanamuziki huyo kumtambulisha bidhaa yake hiyo mpya.

“Kuna siku nilimsihi @MwanaFA na wanamuziki wengine kufanya shughuli nyingine zaidi ya muziki pekee. Nimefarijika leo kunitembelea na kutambulisha bidhaa yake mpya ya “body spray.” Hii ni hatua kubwa na nzuri kwa vijana wetu. Tuwaungishe!” ameandika Dk. Kikwete.

MwanaFA leo amezindua bidhaa yake hiyo inayofahamika kwa jina la Fyn by Falsafa.

About Masalu Erasto

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram