Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Michezo Al Ahly, Zamalek watinga fainal klabu Bingwa
Michezo

Al Ahly, Zamalek watinga fainal klabu Bingwa

Pitso Mosimane
Spread the love

BAADA ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Raja Casablanca, klabu ya soka ya Zamalek imetinga hatua ya fainali ya kombe la klabu Bingwa barani Afrika ambapo itamenyana na mahasimu wao klabu ya Al Ahly. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea).

Mchezo huo wa fainali wenye mvuto wa aina yake utachezwa 27 novemba 2020 kwenye Uwanja wa Borg Al Arab ulipo kwenye mji wa Alexandria nchini Misri.

Zamalek ametinga hatua hiyo kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Raja Casablanca katika michezo ya raundi zote mbili (nyumbani na ugenini) kwenye hatua, huku mahasimu wao klabu ya soka ya Al Ahly ilitinga hatua hiyo baada ya kuifunga Wydad Casablanca kwa jumla ya mabao 5-1 kwenye michezo yote miwili.

Al Ahly ambayo kwa sasa inanolewa na kocha Pitso Mosimane inaingia kwenye mchezo huo wa fainali huku ikiwa haijawahi kufungwa na Zamalek mchezo wowote walipokutana kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika toka mwaka 2005.

Mara ya mwisho timu hizo zilikutana 2013 kwenye hatua ya makundi kwenye michuano ambapo Al Ahly alifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 akiwa kwenye Uwanja wake wa nyumbani.

Ugumu wa mchezo huu wa fainali unakuja mara baada ya Al Ahly kukubali kichapo cha mabao 3-1, kwenye mchezo wa Ligi Kuu nchini Misri dhidi Zamalek katika mchezo uliochezwa 22 Agosti 2020.

Fainal hii inatoa tafsiri ya kuwa klabu hizi za nchini Misri zimeendelea kutawala soka barani Afrika kutokana na uwekezaji mkubwa waliofanya kwenye vikosi vyao katika msimu huu wa mashindano.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!