Ajali ya Ndege

Ajali ya Ndege Serengeti: Wawili wafariki

WATU wawili wamefariki dunia katika ajali ya ndege iliyotokea asubuhi ya leo tarehe 23 Septemba 2019, kwenye uwanja wa ndege mdogo wa Seronera uliko kwenye hifadhi ya Serengeti mkoani Mara. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa ya ajali hiyo imetolewa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Taarifa ya TANAPA inaeleza kuwa, ajali hiyo imetokea baada ya ndege ndogo ya Kampuni ya Auric Air kuanguka katika uwanja wa Seronera.

“Ndege ya Kampuni ya Auric Air imeanguka leo asubuhi katika uwanja mdogo wa ndege Seronera, Serengeti. Rubani mmoja na abiria mmoja wamepoteza maisha. Taarifa zaidi zitatolewa.Rubani na abiria wote ni raia wa Tanzania,” inaeleza taarifa ya TANAPA.

Pascal Shelutete, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Mawasiliano TANAPA amesema ndege hiyo ilikuwa na watu wawili ambao wote wamefariki dunia.

Shelutete amesema, mamlaka husika zitatoa taarifa zaidi juu ya chanzo cha ajali hiyo.

WATU wawili wamefariki dunia katika ajali ya ndege iliyotokea asubuhi ya leo tarehe 23 Septemba 2019, kwenye uwanja wa ndege mdogo wa Seronera uliko kwenye hifadhi ya Serengeti mkoani Mara. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Taarifa ya ajali hiyo imetolewa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kupitia ukurasa wake wa Twitter. Taarifa ya TANAPA inaeleza kuwa, ajali hiyo imetokea baada ya ndege ndogo ya Kampuni ya Auric Air kuanguka katika uwanja wa Seronera. “Ndege ya Kampuni ya Auric Air imeanguka leo asubuhi katika uwanja mdogo wa ndege Seronera, Serengeti. Rubani mmoja na abiria mmoja wamepoteza maisha. Taarifa zaidi zitatolewa.Rubani…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram