Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Ajali ya basi yaua watano, 26 majeruhi Muleba
Habari Mchanganyiko

Ajali ya basi yaua watano, 26 majeruhi Muleba

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi
Spread the love

WATU zaidi ya watano wamepoteza maisha huku 26 wakijeruhiwa katika ajali ya basi iliyotokea leo Ijumaa tarehe 21 Agosti 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kagera … (endelea).

Ajali hiyo imetokea kwenye mteremko wa Kyamalebe wilayani Muleba Mkoa wa Kagera.

Taarifa ya ajali hiyo imetolewa na Revocatus Malimi, Kamanda wa Jeshi  la Polisi mkoani Kagera, wakati anazungumza na wanahabari.

Kamanda Malimi amesema, chanzo cha ajali hiyo ni basi la Kampuni ya  Sabuni lenye namba ya usajili T 392 AZB lililokuwa likielekea jijini Mwanza kupinduka wakati likitokea eneo la Nshamba wilayani Muleba.

Amesema majeruhi wanne kati ya 26 hali zao ni mbaya huku waliosalia wakiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali Teule ya Rubya na Hospitali ya Ndolage.

“Kwa mujibu wa mashuhuda walioshuhudia maiti ambazo tuna taarifa zao ni watano,” amesema Kamanda huyo na kuongeza huko walikopelekwa kwa matibabu yawezekana vifo vikaongezeka

Kamanda huyo wa Polisi amesema, uchunguzi wa awali unaonesha dereva alikuwa mwendo kasi kitendo kilichosababisha  gari kumshinda katika kona ya mteremko huo.

“Uchunguzi wetu wa awali na jiografria ya eneo hili ingawa chanzo cha ajali hakijafahamika, lakini zipo dalili za wazi kwamba kwa vyovyote vile, gari litakuwa mwendo kasi na kona iliyokuwepo hapa,  lilimshinda dereva likapinduka,” amesema Kamanda Malimi.

Amesema Jeshi la Polisi lina endelea kumtafuta dereva wa gari hilo, ambaye baada ya kutokea alikimbilia kusikojulikana.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

error: Content is protected !!